fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Tanzania Teknolojia

HDIF yatenga zaidi ya dola M5 kukuza ubunifu wa teknolojia wa kijamii Tanzania- Taarifa Rasmi

HDIF yatenga zaidi ya dola M5 kukuza ubunifu wa teknolojia wa kijamii Tanzania- Taarifa Rasmi

Spread the love

Miradi 14 mipya imenufaika kupitia uwezeshaji wa awamu ya pili ya mfuko wa uwezeshaji wa ubunifu unaolenga kutumia teknolojia kupata uvumbuzi kwa matatizo ya kijamii.

Mfuko wa uwezeshaji wa HDIF una furaha kutangaza washindi 14 wa awamu ya pili ya uwezeshwaji ambao wanaungana na 23 waliowezeshwa awali.

Fedha hizi za msaada zinatokana na pauni milioni 30 ambazo zimetolewa na shirika la misaada la UKAID kwa ajili ya uwekezaji wa ubunifu Tanzania.

Ili kunufaika na fedha hizi za msaada, taasisi sharti ionyeshe ubunifu, mradi uwe na mchango kwa maendeleo, mradi uwe na mwelekeo unaoeleweka, na uwezo wa taasisi husika kuufanikisha mradi wenyewe.

HIDF-PICHA-TANZANIA

Kwa tathmini ya mfuko wa HDIF, hadi sasa washindi wengi wenye mapendekezo kwenye Nyanja mbali mbali za afya, elimu , maji bora na salama wamejikita zaidi kwenye kusuluhisha matatizo ya afya ya mama na mtoto, ajira kwa vijana na uwezeshwaji na suluhisho za kidijitali.

SOMA PIA  Tujue Kwa Ufupi Historia Ya 'KeyBoard' Na Wapi Tunapoenda Na Teknolojia Hii!

“Watanzania wanasababisha mabadiliko—kwa kutumia teknolojia kuboresha utaratibu wa kutolewa huduma za afya ya mtoto kupitia TotoHealth , kuboresha utaratibu wa maji salama SHIPO na elimu bora kupitia Ubongo Kids,” anasema Afisa mtendaji David B. Mcginty.

Taarifa kuhusu walionufaika wote na fedha hizi za msaada zinapatikana www,hdif-tz.org

Mfuko wa HDIF unatoa chachu kwa vijana wa kitanzania kuwa wabunifu na kutumia teknolojia kuwa fursa ya maendeleo yao wenyewe. “Tangu mfuko wa HDIF uanzishwe mwezi wa tisa 2O13, Tanzania imepaa kwenye orodha ya nchi za teknolojia kutoka 123 duniani hadi 117 kati ya 142 zilizotafitiwa. Ubunifu unahitaji tuwe kijiji ili ufanikiwe,” anasema David B. McGinty.

HDIF pamoja na Tume ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) na UKAID zinafanya kazi kwa pamoja ili kuwezesha wabunifu wa Kitanzania, wajasiriamali , wakereketwa wa maendeleo na wasimamizi wa sera ili kufanikisha maendeleo ya kiteknolojia. Juhudi hizi za pamoja zinalenga kukuza maendeleo ya kijamii.

Wiki ya Machi 13-19 HDIF itakuwa mwenyeji wa Wiki ya Ubunifu (Innovation Week) ambapo mafanikio na changamoto yatazungumzwa. Lengo ni kujifunza na yaliyopita ili kuboresha mfuko na kuwezesha wengi zaidi kuibuka na kunufaika. “Wiki ya Ubunifu inalenga kuwaleta pamoja wale wote wenye miradi na wale ambao wanaweza kuwawezesha,” anasema Joseph Marinakiza, naibu kiongozi wa HDIF. Taasisi zingine zinazohusika na Wiki ya Ubunifu ni Kinu Innovation Hub, Deloitte, Ubalozi wa Finland, Buni Innovation Hub, Tanzania Renewable Energy Incubator, na Ifakara Health Institute.

SOMA PIA  Kuhusu kuzuia makelele ya nje kwenye Google Meet

Mambo ambayo yatagusiwa katika Wiki ya Ubunifu (INNOVATION WEEK) ni “Sauna Safari” ushindani wa ubunifu ambapo washindi wataorodheshwa kwenye programu maalum ya Startup Sauna itakayofanyika nchini Finland mwezi wa tano mwaka huu na Fursa ya kujiunga na Slush 2016. Pia kwenye ratiba ya wiki hiyo ni “Innovation & Design Exhibition” itakayofanyika Nafasi Art Space itakayoshirikisha wabunifu, wasanii na wanasayansi kutengeneza viatu ambavyo haviliwi na wadudu. Ratiba zingine zitakuwa wazi kwa umma ilihali zingine zitakuwa za mwaliko tu. Yeyote ambaye angependa kuhudhuria, tembelea www.hdif-tz.org kujua ratiba ya INNOVATION WEEK TZ 2016.

SOMA PIA  Fahamu Tofauti ya POP na IMAP Katika Barua Pepe!

KUHUSU HDIF

Mfuko wa HDIF unalenga kukuza ubunifu unaoweza kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii katika sekta za afya, elimu , maji safi na salama.

Miradi sharti iwe na mtizamo wa soko la Kitanzania. Mfuko unajikita kwenye kutia mkazo ubunifu, ukuzaji na uendelezwaji wa miradi kwa kushirikiana na wenye miradi wenyewe. Mfuko dhamira yake ni matumizi ya teknolojia kwa maendeleo kuitia suluhisho za changamoto za afya, elimu na maji salama na safi.

Ili kutekeleza azma hiyo Mfuko wa HDIF unajikita kwenye maeneo matatu;

• Msukumo wa ushirikiano baina ya wadau kwenye kuboresha suluhisho zinazoboresha maisha ya binadamu
• Kuwa chachu wa mabadiliko hayo
• Kuleta mabadiliko kwenye takwimu sahihi zinazoweza kupatikana kwa wadau kwenye eneo la maendeleo ya binadamu.Takwimu hizo zitasaidia kwenye kufanya maamuzi husika.

| Chanzo: HDIF |

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania