Inapendeza kuona kampuni inayokupa huduma inakujali sio? na hii haiimaanishi katika kutoa huduma yake tuu iliozoeleka bali hata zile zingine ambazo hatuzitegemei
Mfano kampuni inaweza ikawa inauza maji lakini ukashangaa inatoa mikopo na elimu kwa wananchi licha ya kuwa hiyo sio huduma yake ya kwanza kabisa ambayo ilikusudia kuleta kwa watu. Teknokona inaamini ili kukuwa kwa kampuni na kushamiri lazima kampuni fulani lijiweke karibu na wateja (wananchi) wake.
Hii tunaliona kwa Tigo kwa kushirikiana na ‘Reach for change’ wanakuletea shindano la kipekee la kidigitali. Shindano hili linahusu wale waleta mabadiliko kwa kutumia njia za kidigitali ingawa katika mtandao tigo imesema kuwa mtu yeyote anaweza tuma maombi kwani sio lazima mabadiliko hayo yatokane na udigitali.
“Je, wewe ni mjasiriamali wa kijamii unayefanya kazi ya kuboresha maisha ya watoto na jamii kwa ujumla? Na unatumia vifaa vya tehama kukuza maendeleo yako? Una wazo la kibunifu la kuleta omabadiliko duniani na pia shauku ya kuleta mabadiliko hayo? Shirikisha wazo lako tutekeleze pamoja !” – TiGo
Changamkia hii sasa! Tigo na washiriki wao wa ‘Rich For Change’ wanakuambia kuwa Washindi wa shindano hili watajinyakulia Dola za kimarekani 20,000/- Naam! ni pesa nyingi sana hizi
Wakubwa kwa wadogo kama kichwa chako kina wazo la maana juu ya jambo hili ni muhumu kukimbilia fursa hi, maana mambo kama haya ni machache sana. Fikiria mtu akupe kianzio cha kukamilisha ndoto zako kisa tuu kapenda wazo lako la mabadiliko (maendeleo)
TIGO WANAKUAMBIA
Matumizi ya teknolojia ya digitali yanaweza kuonekana katika namna zifuatazo;
- Kutumia simu,intaneti,na teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA), kama namna moja ya kuchangia suluhu
- Uwezo na kutumia mtandao kwa simu za mkononi, pia TEHAMA kuboresha hali ya maisha na maendeleo ya jamii
- Kupeleka na kukuza upatikanaji wa mawasiliano kwa jamii zilizosahaulika
JIUNGE KATIKA SHIDANO HAPA SASA!
Kwa kubofya ‘Jiunge Sasa!’ hapo juu utaoelekwa moja kwa moja kwenye fomu ya kujaza ili kusonga mbele katika shindano hili.
One Comment