Siku chache zilizopita nilishangaa kupata mfululizo wa updates Facebook nikiambiwa rafiki yangu mmoja ameni’tag’ kwenye video flani. Kuja kuangalia ukurasa wangu wa Profile Facebook ilibidi nianze kazi ya ziada ya kuzifuta video hizo, kwani ilikuwa inaonesha picha ya ngono huku ikisema nitamchukia Rihanna kama niki’click link hiyo kwenda kuangalia hiyo video.
(OMG I Just Hate RIHANNA After Watching This Video[LINK]you will lost your all respect for RIHANNA after watching this)
Jamani hawa ni wezi, wanachofanya ukisha’click ile link wanakupeleka kwenye page nyingine inayofanana na ya Facebook huku wakikudai ufanye mambo mengine kama kuwatumia watu wengine zaidi hata bila ya ridhaa yako. Baada ya hapo akaunti yako itakuwa imetekwa kila uki’log in’ Facebook, kwani kuna vitu vinaitwa ‘cookies’ huwa vinaambukiza Browser yako ya mtandao kama Firefox n.k ziwe zinakurudisha kwenye ile kurasa yao kila utakapo’log in’ Facebook.
Zaidi ya hapo pia zinaiba taarifa zako binafsi kutoka kwenye kompyuta yako na kuzituma kwa watengenezaji wa haya madudu.
Kwa hiyo tafadhari ili usije ukajiaibisha na hata kupoteza heshima yako na hata uwezekano wa kuibiwa taarifa muhimu toka kwenye kompyuta yako, ukiona ‘links’ zenye mambo ya kiwizi wizi na uongo na mara nyingi zinakuwa wanadai wana video za ngono za watu maharufu kama wasanii na waigizaji usiingie mtende!!
Kwa wale ambao akaunti zao zimeathirika wanaweza kutatua kwa ku’uninstall’ browser yao na ku’install’ (Google wanatafsiri ‘install’ kama kupakua, nitajifunza kulitumia) upya. Na baada ya hapo watumie ujumbe marafiki zako wote ambao picha hizi zilisambaa kwa makosa na kuwaomba msamaha.
Nawatakia utumiaji mzuri mitandao ya Kijamii!!!
Nimeandakika makala hii kwa msaada wa;
Google Search,
na
http://www.techparadise.info/2012/05/omg-i-just-hate-rihanna-after-watching.html
Nimeipenda sana