Hapa kuna habari mmoja ambayo ndiyo ya uhakika zaidi nayo ni kwamba Facebook wameanza kutoa ‘App/Software’ ya simu kwa ajiri ya kutusaidia katika ku’share picha tunazopiga kiurahisi zaidi. Kwa sasa software hiyo tayari inapatikana kwa wale wanaotumia vifaa vya Apple kama simu za IPhone na hata IPad tablets.
App/software (‘app’ ndo jina maarufu zaidi siku hizi kwa programu za simu na vifaa vingine kama tablets na kompyuta) hiyo itakusadia wewe katika kupiga picha, ku’tag marafiki zako na kuongeza habari(information) nyingine muhimu kama mahali ulipopiga na mengineyo kabla ya kui’upload kwenda kwenye akaunti yako. Zaidi ya hapo pia itakuwezesha kuona picha za karibuni zilizo’upload’iwa na rafiki zako wa Facebook.
MUONEKANO WA FACEBOOK CAMERA APP KATIKA IPHONE
Na kingine zaidi ni kwamba utaweza ata kuwa una’upload picha nyingi kwa wakati mmoja, hii ni tofauti na kama utataka ku’upload picha Facebook kwa sasa kupitia simu za mkononi, unaweza ku’upload moja moja kwanza, lakini kupitia Facebook Camera app utaweza ku’upload picha nyingi kwa wakati mmoja.
Kwa wale mnaofuatilia habari za teknolojia nje ya Teknokona mtakuwa mmejua kuwa hivi karibuni Facebook wapo katika mchakato wa kununua kampuni ndogo ya Instagram iliyokuwa inamiliki app ya Instagram ambayo inasaidia kupiga picha kupitia vifaa(smartphones) vya Android na Apple, na kuweza kuzituma picha hizo kwenda mitandao mengine ya kijamii kama Facebook na Twitter. Kwa hiyo kulikuwa hamna sababu ya kumiliki apps mbili zitendazo kazi moja. Kwa hiyo maswali katika wengi ni je kwa nini Facebook imetumia dola za Kimarekani bilioni moja kunua app ambayo wanaweza kutengeneza, lakini sasa nadhani jibu lipo wazi…wanataka kila tutumiacho kwa simu zetu tuwaze Facebook, na zaidi ya hapo hii ni sawa na kumiliki makampuni mawili yatumiwayo zaidi na watu, unakuwa unahakika wa mapato! Kupitia watumiaji wa Facebook zaidi ya milioni 800 kuna soko zuri la matangazo hasa ukichukulia watu wengi zaidi hutumia mtandao huu kupitia simu za mkononi.
Habari za chini ya kapeti kupitia mtandao mmoja ni kwamba Facebook wanataka kuinunua Opera, kampuni itengenezayo browser ya Opera kwa ajili ya kompyuta na OperaMini maarufu kwa ajili ya simu. Kama habari hizi ni za kweli nadhani tunaona Facebook ikitaka kujikuza zaidi katika ushindani na kampuni kama Google, ambayo inamiliki Chrome browser na pia mtandao wa kijamii wa Google+.
Yetu macho, kama habari hizi zitathibitishwa nitawatonya..
No Comment! Be the first one.