fbpx
Facebook, Intaneti, Maujanja, Mtandao wa Kijamii

Facebook: Kubadilisha nywila (nenosiri) inawezekana!

facebook-kubadilisha-nywila-nenosiri-inawezekana
Sambaza

Inawezekana tangu ufungue akaunti ya Facebook hujawahi kufikiria kubadilisha au hata kufanya jitihada na hatimae kuweza kubadilisha nywila na kuweka nyingine iliyo imara na madhubuti kwa usalama wa taarifa zako na mambo mengine kwenye Facebook.

Si vizuri kabisa utumie nenosiri hilohilo kwa muda mrefu sana kutokana na sababu za kiusalama na ili kuepuka udukuzi ambao kwa asilimia kubwa unaweza kuepukwa iwapo ukiwa na tabia ya kubadilisha nenosiri mara kwa mara.

INAYOHUSIANA  Tumia Simu Yako Kama Vifaa 10 Tofauti Vya Ki-elektroniki!

Hatua za kufuta ili kubadilisha nywila kwenye Facebook.

 1. Ingia kwenye mpangilio (settings) kwenye Facebook. Katika masuala mbalimbali kama vile kubadilisha jina, nenosiri, n.k kwenye mpangilio ndio hatua ya kwanza kabisa na itakayokuwezesha kuweza kubadilisha/kurekebisha kulingana na vipengele vilivyopo.

  Kubadilisha nenosiri kwenye Facebook: Kwenye mpangilio ndani ya Facebook ndio uti wa mgongo wa kile ambacho unatarajia kwenda kufanya baada ya ukurasa mwingine kufunguka.
 2. Bofya kwenye kipengele cha Security and Login. Hii ndio hatua ambayo itafanikisha lile lengo lako la kutaka kubadilisha nenosiri ambalo pengine hujawahi kubadilisha tangu uwe na akaunti ya Facecook au una tabia ya kubadilisha nywila ya kwenye Facebook kila baada ya muda fulani.
  Kwenye kipengele cha Security & Login ndio sehemu ya kuangalia mambo tofauti tofauti kuhusu ulinzi wa akaunti yako ya Facebook.

  Ukiwa ndani ya kipengele cha Security & Login moja kwa moja kwenye ‘Change password‘ na hapo utaweka nenosiri la sasa kisha chini yake utaweka nenosiri jipya na kurudia nenosiri lile katika kipengele kinachofuta.

Hitimisho la zoezi zima la kubadilisha nenosiri kwenye Facebook ni kukukumbuka kuhifadhi (save) kile ambacho umekifanya. Kubadilisha nywila si kitu kigumu lakini ni vyema ukawa na kumbukumbu ya lile nenosiri jipya utakalokuwa unatumia baada ya kubadilisha nywila ya zamani.

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

 1. Facebook: Kubadilisha nywila (nenosiri) inawezekana! – TeknoKona Teknolojia Tanzania
  January 22, 2018 at 6:46 pm

  […] post Facebook: Kubadilisha nywila (nenosiri) inawezekana! appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

 2. Namna ya kufunga nyaraka kwa nenosiri - TeknoKona Teknolojia Tanzania
  May 19, 2020 at 2:16 pm

  […] Usalama kwenye maisha yaliyotawaliwa na teknolojia ni kitu muhimu sana hasa pale unapopenda kuwa mtu wa kutopenda kuweka mambo yako wazi na katika zama hizi za kidijitali matumizi ya nenosiri si jambo la ajabu. […]