fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone simu Uchambuzi

iPhone SE: Simu ya ‘bei nafuu’ zaidi Kutolewa na Apple?

iPhone SE: Simu ya ‘bei nafuu’ zaidi Kutolewa na Apple?

Spread the love

Apple wametambulisha simu yao mpya ya iPhone SE, ambayo imepata sifa ya kuitwa simu ya bei nafuu zaidi kuwahi kutolewa na Apple. Nafuu???? Si wote watakubali… 😀

Katika utambulisho wa simu hiyo uliofanyika jana nchini Marekani toleo la simu ya iPhone SE linalenga kuzidi kuongeza mauzo ya simu za iPhone katika masoko ya nchi zinazoendelea na ata zile zilizoendelea ambazo watumiaji flani wanaona matoleo kama iPhone 6S na iPhone 6S Plus ni ghali sana.

SOMA PIA  Jinsi Ya Kulazimisha MacBook Ijae Chaja Asilimia 100 Kwa Uharaka!

Pia inasemekana uamuzi wa iPhone kuanza nao kutoa simu zenye maumbo makubwa kama vile kwa Samsung kuliwaaudhi baadhi ya wateja wao wasiopenda simu zenye maumbo makubwa.

iPhone SE

Inasemekana SE kwenye iPhone SE inasimama kwa ‘Special Edition’, yaani toleo maalumu.

Bei?

Simu ya iPhone SE itaanza kupatikana kwa dola 399 za marekani (Tsh 875,000/= | Kes 40,500/=) kwa toleo la GB 16 na huku la GB 64 litapatikana kwa dola 499.

Sifa za iPhone SE

iPhone SE

  • Ina teknolojia za 2G, 3G na LTE – WiFi
  • Chipi ya A9 – 64Bit
  • Ukubwa wa inchi 4
  • Kamera ya Megapixel 12 (f/2.2, 29mm, autofocus, dual-LED (dual tone) flash)
  • Inasemekana ndani yake ina RAM ya GB 2
SOMA PIA  Mambo Ambayo Steve Jobs Alisema Kamwe Apple Hawatayafanya na Wanayafanya Sasa!

Kwa kifupi iPhone SE ni simu janja yenye umbo dogo ila yenye uwezo mkubwa sana. Suala la bei bado wengi wanaona ingawa ni bei ya chini ukilinganisha na matoleo mengine ila bado ipo juu – ‘ila ndio hivyo tena, kitu tayari kinaitwa iPhone’, lazima bei iwe ghaghariiii a.k.a Ndi Ndi Ndi 🙂  😀

iPhone SE kushoto ikiwa pamoja na iPhone 6S, 6S Plus, 6 na 6 Plus

iPhone SE kushoto zikiwa pamoja na iPhone 6S, 6S Plus, 6 na 6 Plus

Inasemekana watu wengi hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, India n.k waliokuwa wanatamani kumiliki simu mpya kabisa ya iPhone wataweza kufanya hilo kwa mara ya kwanza. Kwani ingawa ina umbo dogo, bado ni simu inayovutia na inayopatikana kwenye bei iliyo chini ukilinganisha na matoleo mengine.

SOMA PIA  Simu janja Nokia G11 yazinduliwa bila matangazo

Simu hii itaanza kupatikana kuanzia mwisho wa mwezi wa tatu mwaka huu. Tuambia mtazamo wako juu ya ujio wa iPhone SE kupitia eneo la comment.

Picha na PocketNow na Techradar

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] Toleo hili la simu ya SE ambalo limezinduliwa jana ni toleo ambalo limetengenezwa kwaajiri ya watumiaji ambao hawapendi simu zenye ukubwa kama wa iPhone 6 ama 6s lakini wanapenda uwezo wa simu hizi sa sasa. Soma uchambuzi wa iPhone SE hapa -> Uchambuzi: iPhone SE […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania