Unaweza ukawa unajiuliza mbona jambo hili limefanikiwa mara baada ya muda mchache tuu kupita tangia iPhone 14 ilipoingia sokoni…

Kampuni ambayo imekua ni mshirika mkuu wa uzalishaji wa vifaa vya iPhone kwa muda mrefu, Foxconn inadai kuwa ina kiwanda cha kufanya hivyo karibu na jiji la Chennai huko india na kwa sasa wananza na iPhone 14.
Apple ni moja katika makampuni makubwa yanayozalisha na kuuza simu janja, kwa kipindi cha muda mrefu wameweza kushinda mioyo ya wateja wao maana kwa sasa ni baadhi ya kampuni ambayo inauza simu nyingi sana ukilinganisha na makampuni mengine
Kingine ni kwamba katika mategemeo ya Apple ni kwamba mpaka kufikia mwaka 2025 inatarajia kuwa India iwe ni moja kati ya nchi kuu zinazozalisha vifaa vya Apple.
Kingine kinachojulikana ni kwamba kwa harakaharaka ni kwamba kampuni inahamisha asilimia 5 za uzalishaji wa iPhone 14 huko India mpaka mwishoni mwa mwaka huu.

Na mpaka kufikia mwaka 2022 inategemewa kampuni kuweza kuzalisha asilimia 25 ya iPhone Zote (zitakazokuwa zinazalishwa) mpaka kufikia mwaka 2025.
Kwa sasa ni jambo la kawaida sana kwa baadhi ya makampuni yanayojihusisha na uzalishaji wa bidhaa kuwa na viwanda katika maeneo tofauti tofauti, sababu kubwa ikiwa ni kupunguza gharama na kufikia wateja kiurahisi kabisa n.k
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa kampuni kuanzisha viwanda maeneo mbalimbali? Au wangebaki kule china tuu??
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.