fbpx
Apple, IPad, simu, Teknolojia, Uchambuzi

iPad Pro ya mwaka 2020 ndio hii

ipad-pro-ya-mwaka-2020-ndio-hii
Sambaza

Mwaka huu Apple wameamua kuirudisha tena iPad Pro ikiwa na maboresho kadha wa kadha na mtangullizi wake alitoka mwaka 2018.

Mwezi Machi 2020 toleo jipya la iPad Pro kwa mwaka husika imetoka huku ikionekana ikiwa na maboresho kadha wa kadha kulingana na ilivyowapendeza wao lakini hata mahitaji ya soko pia. Yapo mengi ambayo nitayaangazia lakini nianze tuu kwa kusema kifaa hicho hakina teknolojia ya 5G!.

Kwenye toleo hili jipya Apple wameboresha upande wa kipuri mama, kamera lakini kiujumla muonekano wake ni sawia na mtangulizi wake-iPad Pro 2018. Sifa zake ni kama ifuatavyo:-

INAYOHUSIANA  Mswada wa matumizi ya simu kwa watoto

Kipengele

iPad Pro 2020

Kioo Kioo kina urefu wa inchi 12.9 (2732 x 2048 pixels) Liquid Retina LED-backlit IPS display.
Muonekamo Inafanana sana na iliyotangulia isipokuwa toleo la sasa ni pana kidogo.
Kipuri mama Inatumia A12Z Bionic
mwaka 2020
iPad Pro ya mwaka 2020.

Kipengele

iPad Pro 2020

Kamera

Nyuma: Kamera mbili-MP 12 na MP 10+LiDAR sensor-ni mahususi kwa teknolojia ya Augmented Reality (AR).

 

 

 

 

Mbele: Ina kamera moja yenye MP 7+Face ID.

RAM/Diski uhifadhi
 • 6GB za RAM kati ya GB 128 au TB 1 memori ya ndani.
Betri
 • 9720mAh ndio nguvu ya betri.
 • 18W teknolojia ya kuchaji haraka
 • Inadumu na umeme kwa muda wa saa 10
INAYOHUSIANA  Huawei P9: Huawei waomba radhi baada ya kupost 'uongo'!
mwaka 2020
Muonekano wa kamera za nyuma na ile ya mbele.

Kipengele

iPad Pro 2020

Bei

 • $799| zaidi ya Tsh. 1,837,700 (GB 128),
 • $899| zaidi ya Tsh. 2,067,700 (GB 256),
 • $1,099 | zaidi ya Tsh. 2,527,700 (GB 512) na
 • $1,299| zaidi ya Tsh. 2,987,700 (TB 1).

Rangi

Fedha na Kahawia.

Mengineyo

 • Inatumia WiFi, 4G/LTE pia nyingine unaweza ukaweka kadi ya simu,
 • Ina iOS 13.4, inatumia kicharazio kinachogharimu $349|Tsh.802,700 na kalamu ipo,
 • Uzito ni 641g (Wi-Fi), 643g (4G),
 • Inatumia Type-C 3.1,
 • Ina kitufe cha kutembea huku na kule (trackpad)/kicharazio cha mguso.
INAYOHUSIANA  Gemu la Snake (Nyoka) Linakuja Kwenye Simu Janja
mwaka 2020
Ung’avu wa muonekano wa kitu kwenye toleo hilo jipya.

Kiujumla toleo la iPad 2020 si bora sana kuzidi mtangulizi ingawa ina kipuri mama chenye nguvu zaidi, ukubwa wa RAM kuzidi iliyopita lakini mbaya zaidi ni ghali kulinganisha na ile iliyopita.

Vyanzo: MacRumors, Pocket Lint

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

1 Comments

 1. Uundaji wa iPhone 12 unaendelea kama kawaida - TeknoKona Teknolojia Tanzania
  March 29, 2020 at 11:10 am

  […] iPad Pro ya mwaka 2020 ndio hii […]