fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Huawei Samsung simu Xiaomi

Samsung yaongoza Mauzo ya Simu, Huawei wazidi Kuporomoka

Spread the love

Huawei wazidi kuporomoka kimauzo katika soko la uuzaji simu duniani. Data zinaonesha Samsung wakizidi kulishika soko huku Huawei mambo yakienda tofauti kwao.

Data za kimauzo zinlizotolewa na shirika la utafiti masoko la Counterpoint Research zinaonesha kwa mwezi Agosti mwaka huu Samsung walishika asilimia 22 ya mauzo yote ya simu janja duniani. Hii ni nafasi ya juu ukilinganisha na mwezi wa Aprili mwaka huu ambapo mauzo yao yalikuwa asilimia 20 na huku Huawei alikuwa namba moja akishika soko la simu janja kwa asilimia 21.

huawei wazidi kuporomoka kimauzo

Samsung yaongoza Mauzo ya Simu, Huawei wazidi Kuporomoka

 

SOMA PIA  Simu janja za Android ni nyingi lakini si zote zitakazopata sasisho la Android P

Kutoka ushikaji soko wa asilimia 21 mwezi wa nne, hadi asilimia 16 mwezi wa nane mwaka huu hili ni anguka la asilimia kubwa kwa Huawei na linahusishwa moja kwa moja na vikwazo vya kibiashara ambavyo imewekewa na Marekani.

Xiaomi ndio moja ya kampuni inayonufaika zaidi pia na hali hii ya Huawei ambapo nafasi yao kimauzo imepanda kutoka asilimia 8 mwezi wa nne hadi kufikia asilimia 11 mwezi wa nane. Kwa wanunuaji wengi wa simu hasa wa barani Ulaya, Xiaomi inaonekana kama ndio kampuni nyingine ya kichina inayoweza kuaminika zaidi kwenye ubora wa simu zake na huku apps za Google na soko lake vikiwa vinapatikana kwenye simu hizo.

huawei p40 Pro

Ingawa kuna simu nzuri Huawei wametambulisha mwaka huu ila soko la nje ya China hazijafanya kimauzo kutokana na kutokuwepo kwa apps mbalimbali muhimu kwa watumiaji wa kimataifa, hii ni Huawei P40 Pro

Je una mtazamo gani juu ya anguko hili la Huawei? Je wewe unaweza kununua simu ambayo haina uwezo wa kuwa na apps mbalimbali muhimu kama vile Facebook, Google, Soko la Google Play, Instagram, WhatsApp na zingine nyingi kwa kuwa tuu ni simu nzuri kutoka Huawei?

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania