fbpx

Herufi zenye maana kubwa sana kwenye kicharazio zaidi ya kazi zake

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Simu zimetapakaa mijini na vijijini na tunazitumia kila leo katika shughuli zetu za kila siku lakini unaweza ukawa unatumia kitu mara kwa mara na usijue kina maana gani.

Ukiangalia kwenye kicharazio (keyboard) utaona ina vitufe vingi ambavyo vinafanya kazi ya kufanikisha kazi zako kwa kile unachokiandika lakini kama ni mtu unayependa kujua vitu lazima utakuwa umeshawahi kujiuliza “Kwanini namba 5 (ya kwenye simu) kwenye kicharazio kinachoshikika ni tofauti na nyingine?” au “Vitufe F na J kwenye kicharazio cha kwenye kompyuta zina utofauti unaofanana ukizishika?“.

Kwanini namba tano (5)  kwenye simu za kawaida imezungukwa na nukta mbili?

Ukweli ni kwamba kwa mtu ambae ana uwezo wa kuona hawezi kujua siri/maana kubwa ya zile nukta ndogo ambili ambazo utazionaupande wa juu/chini ama kulia au kushoto wa namba tano lakini:

Kwa mlemavu wa macho (mwenye huoni hafifu/haoni kabisa) zile nukta mbili zina maana kubwa sana kwake na kuashiria kuwa kidole chake kipo katikati hivyo kutokea pale anajua kuwa kwenda juu atagusa namba 2, kwenda chini ipo namba 8, n.k.

maana kubwa sana

Nukta hizo mbili karibu na namba 5 ndio mwongozo wa mlemavu wa macho pale anapotaka kupiga simu.

Je, mambo ni sawa kwa vitufe F na J kwenye kicharazio cha kwenye kompyuta?

Wakati mtu anataka kujifunza kuwa na kasi wakati anaandika kwa kutumia kicharazio cha kwenye kompyuta ni lazima atajifunza jinsi ya kupanga vidole vyake vya mkono wa kulia na kushoto lakini zile alama unazoziona kwenye herufi F na J zina maana ya kwamba kidole cha pili cha upande wa kushoto (baada ya dole gumba) kikae kwenye herufi F na kidole cha pili baada ya gumba la mkono wa kulia kikae kwenye herufi J.

maana kubwa sana

Vidole hivyo viwili vikikaa sehemu yake hutakuwa unakosea wakati wa kuandika vitu kupitia kicharazio.

Kwa mlemavu wa macho na ambaye kumiliki simu janja ni changamoto basi yenye zile nukta ndio msingi na mwongozo wake wakati wa kutaka kufanya kitu kwenye simu.

Daima panga vidole vyako kwenye sehemu yake hasa vile vidole viwili na ukienda kinyume na hapo lazima utakosea tu.

Vyanzo: Quora, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Huawei P30: Hizi hapa simu mbili mpya za Huawei za P30 na P30 Pro
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.