Mabadiliko ya teknolojia yanaweza kufanya watu/makampuni kushirikiana na mwisho wa siku wakatengeneza/kuunda kitu ambacho kitawanufaisha wengi na mwisho pande zilizoshirikiana kunufaika.
Wengi wetu kama si wote tunafahamu kuwa unaweza kutumia WhatsApp kwenye kompyuta (WhatsApp Web) lakini hii ikimaanisha lazima yawepo mawasiliano kati ya simu janja na kompyuta huku kiunganishi kati yao kikiwa ni intaneti.
Pengine hilo suala likabadilika na watu wakaacha kutumia WhatsApp Web kwani inaaminika kuwa Microsoft na WhatsApp wanafanya kazi kwa pamoja kuweza kuleta WhatsApp ya kwenye kompyuta. Hii ikimaanisha kuwa hatukwa na haja ya kutumia WhatsApp Web ili kuweza kutumia programu hiyo kwenye kompyuta.
Ushirikaino kati ya WhatsApp na Microsoft umesukumwa na nini?
Kwa ambao wameshawahi kutumia/wanatumia mara kwa mara WhatsApp Web wanafahamu ya kuwa huwezi kupiga simu ya kawaida au kwa njia ya picha jongefu kupitia njia hiyo ya kutumia WhatsApp kupitia kompyuta.
Pili, Microsoft wana lengo la kuifanya WhatsApp wanayoitengeneza iweze kwenye kazi bila shida yoyote kwenye vifaa vinavyotumia Windows lakini pia hata kwenye programu endeshi ya Windows 10.
WhatsApp ya kwenye kompyuta itasaidia matumizi ya simu ili kuweza kutumia programu hiyo lakini pia kiwango cha intaneti ambacho kinatumika kwenye simu na kwenye kompyuta ili kuweza kutumika.
Vyanzo: Gadgets 360, Windows Central, TnW
One Comment
Comments are closed.