fbpx
simu, Teknolojia, Usalama

Teknolojia ya Fingerprint yashindwa kufanya kazi kwenye baadhi ya simu za Samsung

fingerprint-yashindwa-kufanya-kazi-samsung-galaxy-s10-na-note-10

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Teknolojia ya Fingerprint yashindwa kufanya kazi kwa usahihi kwenye baadhi ya simu maarufu za Samsung.  Apps za huduma za kibenki zaanza kuzuiwa kufanya kazi.

Mabenki katika mataifa kama Uingereza, Marekani na China yaondoa apps zake kwenye simu za Samsung Galaxy S10 na Note 10 baada ya tatizo la kiusalama linalohusisha uwezo wa kufungua simu kw alama za vidole (fingerprint).

bei ya samsung galaxy s10
Muonekano: Samsung Galaxy S10e, Galaxy S10 na Galaxy S10 Plus

Kwa takribani wiki sasa imefahamika teknolojia ya kisasa inayotumika kwa ajili ya kutambua alama za vidole kwa simu za Galaxy S10 na Note 10 inaweza kujikuta ikikubali vidole ambavyo si sahihi au vya watu wengine kimakosa.

Apps za mabenki zimekuwa zikitengenezwa zikitegemea mfumo wa teknolojia ya utambuaji alama za vidole, mabenki yamechukua uamuzi huu kuepusha watu kuibiwa pesa iwapo watu wasiohusika wakiweza kuzifungua simu za wateja wao kutokana na tatizo hili.

INAYOHUSIANA  TCRA: Utumiaji Wa Simu Feki Umeshuka!

Hilo limefahamika baada ya watumiaji kadhaa ambao walitumia viulinzi kioo – screenprotectors kwenye simu zao na wakajikuta mfumo huo wa ufunguaji kwa alama za vidole ambao upo kwenye kioo/display kujikuta haufanya kazi vizuri.

Teknolojia ya utambuaji alama za vidole kwa mfumo wa kugusa kioo (display) ndio teknolojia inayopendwa kwa sasa ili kuachana na teknolojia ile ya kuweka eneo spesheli hasa hasa nyuma ya simu.

INAYOHUSIANA  Fanya Kompyuta Yako Iweze Rusha WiFi Kwa Vifaa Vingine!

mfungo wa fingerprint note s10 Fingerprint yashindwa kufanya kazi

Samsung wameshakubali uwepo wa tatizo hilo, wamehaidi kuleta sasisho jipya la programu endeshaji katika simu hizo ili kuondoa tatizo hilo. Tatizo hilo limekuwepo kwa watu wanaotumia screenprotector tuu.

Kama unatumia simu ya Samsung Galaxy S10 na Note 10 kwa sasa basi fahamu kama umeiwekea screenprotector basi kuna uwezekano wa zaidi ya asilimia 50% mtu mwingine kuweza kuifungua kwa alama ya vidole. Unashauriwa kuuzima uwezo wa fingerprint kwa sasa, Samsung wamesema ndani ya wiki moja watakuwa wameshatoa sasisho(update) la kurekebisha hilo.

Vyanzo: GSMArena
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |