Kwa dunia ya sasa kuna mitandao mingi sana ya muziki tena ile ya ku’stream, mitandao hii ipo ambayo ni ya kulipia na ile ya bure kabisa.
Kuna mitandao mingi ambayo inatoa huduma hii ila ile maarufu ni kama Apple Music, Spotify, Amazon Music, Tidal, Deezer, YouTube Music— na mingine mingi tuu ambayo inatoa huduma ya muziki wa ku’stream.
Lakini katika mitandao yote hii ambayo ina majina makubwa, je ni upi ambao una nyimbo nyingi kushinda mitandao mingine?
Hapa tutaangazia katika mitandao mikubwa ile 7 tuu
Apple Music
Amazon Music
Deezer
SoundCloud
Spotify
Tidal
YouTube Music.
- SoundCloud: ina nyimbo milioni 300+
- Apple Music: ina nyimbo milioni 100+
- Amazon Music, Tidal, na Deezer: ina nyimbo milioni 90+
- Spotify and YouTube Music: ina nyimbo milioni 80+
Namba hizi zinajumuisha nyimbo tuu na kuachana na vitu vingine vingi ambavyo vinapatikana katika mitandao hii kama vile podcast na mambo mengine mengi
Mtandao wa Spotify ndio mtandao maarufu katika kutoa huduma hii na una wafuasi/watumiaji wengi ukilinganisha na mitandao mingine lakini pia cha kushangaza ni kwamba una nyimbo chache.
Kinigine ni kwamba mtandao kama Soundcloud sawa una nyimbo nyingi lakini ukifikiria kiundani miziki mingi katika mtandao huo haina ubora kama katika huduma zingine (mfano spotify).
Ningependa kusikia kutoka kwako, je ni mtandao gani ambao unautumia kusikiliza sana muziki? Je hukubaliani na namba hizi? Tuandikie hapo chini ya comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.