Kampuni ya Apple imefanya mabadiliko tena baada ya kurudisha mitandao miwili mmoja ukiwa ni wa kijamii, VKontakte na mwingine ukiwa ni wa maswala ya barua pepe (E-mail) unaojulikana kama Mail.ru
Haya ni makampuni makubwa sana (VK au Vkontakte na Mail.ru) huko nchini urusi na ilitokea yakapigwa marufuku katika soko la App la App store.
Hii ikiwa ni moja kati ya sababu za kiserikali kati ya Urusi na serikali ya uingereza (uingereza kuruhusu/kukataza baadhi ya vitu/mambo kutoka urusi)
Tangia jambo hili kutokea (kutolewa) kwa sasa zimepita wiki tatu ndio App hizo zinarudhiswa katika soko la Apple.
Mitandao hiyo miwili ni mikubwa kama vile Facebook na Gmail huko nchini urusi (kwa warusi wengi) na iliingia katika seke seke hilo baada ya serikali ya uingereza kuingilia kati
Mpaka sasa Apple bado hawajaweka sababu ya juu kwanini wamerudisha App hizo katika soko lao maarufu la App Store.
Mtandao wa VK ulianzishwa mwaka 2006 na bwana Pavel Durov ambae pia ni muasisi wa kampuni na mtandao wa kijamii wa Telegram, pengine hapo utapata picha kidogo jinsi mtandao huo ulivyo na nguvu.
Lakini sababu ambayo vyombo mbalimbali vinasema ni kwamba wanadhani haya yote yametokea kwasababu App hizi zinasambazwa na waandaaji au zinamilikiwa na pande ambazo zimewekewa vikwazo vikali na serikali ya uingereza.
Kwa sababu ya hapo juu, bado watu wanabaki midomo wazi kwani tangia kuondolewa kwake mpaka kurudshwa hakuna umiliki wowote wa mitandao hiyo uliobadilika.
Kingine ni kwamba App kama VK inasadikiwa kupata mkono/uhusiano katika bank ya Gazprombank ambayo viongozi wake wa juu waliwekewa vikwazo vikali na serekali ya uingereza.
Mpaka sasa bado kuna vikwazo katika bank ya Gazprombank na serikali ya uingereza na kama nilivyosema hapo juu hata Apple hawajatoa sababu za kurudisha App hizo.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.