fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Teknolojia

Fahamu Kuhusu KeyBoard Ya Emoji Kutoka EmojiWorks!

Fahamu  Kuhusu KeyBoard Ya Emoji Kutoka EmojiWorks!

Spread the love

Je umekua ukiwa una hamu na njia rahisi ya kukuwezesha kutuma Emoji? Hilo linaweza kuwa sio tatizo tena kwani ufumbuzi umepatikana. Katika ujumbe/meseji zetu za kila siku sio rahisi kihivyo kupata Emoji tunazozitaka kwa muda huo kwa haraka zaidi kwani ni lazima tuingie katika chumba cha Emoji na kisha tuchague ile tuanyotaka kuitumia kwa kuibofya mara moja, mbili, tatu na kuendelea.

Wengine wanaona shida mara kwa mara kuingia katika chumba cha kutafuta Emoji mpya hivyo wanakuwa na Emoji zao ambazo wanazitumia mara kwa mara. Wengi wetu nna wasiwasi hata hatufikishi asilimia 40 ya matumizi ya Emoji zote zilizopo kwenye vifaa vyetu

Keyboard Ya Emoji Kutoka EmojiWorks

Keyboard Ya Emoji Kutoka EmojiWorks

Hebu fikiria mfano katika App ya WhatsApp umeshawahi kumaliza hata kutumia 14 ya Emoji hizo? au kila siku unatumia Emoji zako katika sehemu ya zile unazozitumia sana ‘Favourite’

Kampuni linalojulikana kama EmojiWorks kutoka Austin limekuja na ukombozi kwa watu wanaopenda kutuma Emoji katika ujumbe au hata meseji zao Kwa kuleta ‘KeyBoard’ ambayo imepambwa na Emoji mbalimbali. Kampuni hili limefanya hivi makusudi ili kusaidia watu waweze kutuma Emoji hizo kwa haraka na wasipoteze muda kwa kubofya vibonyezo mbalimbali ili mradi tuu itokee EMoji wanayotaka.

Kuandika Emoji kwa kutumia shotikati pia inaleta shida saa zingine kwani ni vigumu kukumbuka njia hizo kwa kila Emoji na pia itakubidi kutumia muda wako mwingi katika mtandao ilimradi tuu upate kizishika njia hizo.

SOMA PIA  Afrika yapata utambulisho wake(".africa") baada ya miongo mitatu

Pengine hii inaweza ikiwa sio Keyboard pekee ya Emoji lakini ni keyboard ambayo ina umbo sawa na keyboard za kawaida na pia inaweza ikanunulika tuu — Zingine ni mtihani —  (hah!)

Pia unaweza kutumia Keyboard hii kwa kuandika maneno ya kawaida tuu kwani katika kila kibonyezo cha Keyboard hii kuna neno moja  na Emoji tatu. Itakubidi Umebonyeze kibonyezo cha ‘Emoji’ sambamba na Emoji unayotaka katika kitufe chake husika.

SOMA PIA  Amazon wanasuka mpango wa "Nunua sasa lipa baadae"

EmojiWorks wanasema kwa kutumia keyboard yao utasevu muda wako mara kumi na si hivyo tuu bali pia wameongeza Emoji mpya zilizoingia mwezi septemba.

Keyboard hii ni moja kati ya zile za kuunganisha kwa kutumia Bluetooth na kuna matoleo matatu. Tofauti za matoleo hayo ni wingi wa Emoji mtumiaji anazotaka katika Keyboard.

Je wewe ni mtumiaji mzuri wa Emoji na stika mbalimbali? tuandikie nini umekipenda kuhusu makala hii. Emoji tunazitumia kwa sana namara nyingi zinaleta hisia nyingi kuliko maneno ya kawaida. Pia usisahau kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na miujiza mingine ya Teknolojia. TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] post Fahamu Kuhusu KeyBoard Ya Emoji Kutoka EmojiWorks! appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania