fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao

Mtandao Wa Jay-z (Tidal) Kuongeza Michezo Ya Kuigiza Katika Huduma Zake!

Mtandao Wa Jay-z (Tidal) Kuongeza Michezo Ya Kuigiza Katika Huduma Zake!

Spread the love

Ili kuendele kujitofautisha na mitandao mingine ya kulipia ili kusikiliza musiki katika mitandao, mtandao unaomilikiwa na mwana Hip Hop wa kimataifa (Jay-z) wa Tidal umeongeza huduma. Huduma hii haikutegemewa na watu wengi na imekuwa ya kushtua kwa baadhi ya watu pia.

Mpaka sasa tidal ina watumiaji wa kudumu zaidi ya milioni moja, Ina zaidi ya video za musiki 86,000 pia ina miziki zaidi ya milioni 38.

Jay-z

Jay-z

Watu wengi walitegemea mambo kadha wa kadha kutoka katikia miziki (video na audio) kupitia mtandao huo wa tidal. Lakini Tidal nao pia walikuwa na mawazo yao. Hivi sasa tidal itaanza rasmi kuonyesha michezo ya kuigiza (Tv Series) katika mtandao wake. Michezo hiyo itakua ya aina mbili yaani ule uliondikwa na ule usio wa kuandika (Kutofautiana katika Script) Michezo hiyo ikiwa ni Money & Violence na No Small Talk

Tidal imetoa oda ya msimu wa pili wa mchezo wa Money & Violence ambao mara ya kwanza ulikua ukionyeshwa katika mtandao wa Youtube. Mchezo huo uliandaliwa na kuchezwa na Moise Verneau. Series hii inaelezea vijana wanoishi katika maisha ya tabu huko Brooklyn ambao wanakuja kuwa wezi na kujihusisha katika madawa ya kulevya. Hili lilimgusa Jay-z kwa sababu nae alizaliwa na kukulia Brooklyn pia.

Series Ya Money & Violence

Series Ya Money & Violence

Msimu wa pili (season 2) wa Money & violence utaanza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza katika mtandao wa Tidal januari mosi mwakani. Kwa sasa Tidal wanaonyesha msimu wote wa kwanza katika mtandao wao ili watu wapate na wazo juu ya nini kinakuja na pia hata kupata baadhi ya mawazo ya watumiaji wa mtandao huo.

No Small Talk Inasimamiwa Na Dj  maarufu, Cipha Sounds

No Small Talk Inasimamiwa Na Dj maarufu, Cipha Sounds

Mchezo wa kuigiza wa pili ambao tidal itaongeza katika listi yake ni ule unaojulikana kama No Small Talk ambao unasimamiwa na Dj maarufu, Cipha Sounds. Msimu wote utakuwa na sehemu (Episode) tano na kila sehemu itakuwa na takribani ya muda wa nusu saa.

SOMA PIA  50 Cent Aamua Kuikacha Instagram

Mamuzi ya kuongeza michezo ya kuigiza katika mtandao yamekuja baada ya kampuni kuona kuwa inabidi watu waweze kupata huduma nzuri ya pesa zao wanazozitumia katika mtandao. Tuandikie katika sehemu ya comment hapo chini, maamuzi haya unayachukuliaje ukilinganisha na mitandao mingine? Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku kwani TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Comments

  1. […] post Mtandao Wa Jay-z (Tidal) Kuongeza Michezo Ya Kuigiza Katika Huduma Zake! appeared first on […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania