WhatsApp ni moja kati ya mtandao wa kijamii ambao ni maarufu sana na unapendwa sana na watu. Mtadnao huu hutumiaka kama sehemu ya mawasiliano ya haraka.
Ni mara kadha wa kadha mtandao huu –wa WhatsApp– huwa unatoa masasisho (update) mpya na sasa imekuja na kipengele ambacho kinakurahisishia katika swala zima la kujitumia meseji.
Kuna muda mtu unatamani kabisa kujitumia kitu katika mtandao wa WhatsApp lakini unashindwa sababu kipengele hiki hakikuwepo.
Pia hii inakua ni kama sehemu yako ya kuhifadhi baadhi ya vitu vyako kama vile nyaraka n.k. Kipengele hiki kampuni imekipa jina la Jitumie meseji mwenyewe (Message Yourself).
Ni wazi fununu ya kipengele hiki zilianza nyuma kidogo, japokuwa kwa wengi itakua sio kipengele cha kuwashangaza sana maana kuna njia nyingi za kuhifadhi vitu vyako vya muhimu katika vifaa vyetu sio?
Kwa sasa kipengele hiki bado kipo katika hatua ya kuachiwa na kwa sasa kinaendelea kuachiwa zaidi kari muda unavyozidi kwenda.
Kwa sasa hakikisha una toleo jipya kabisa la mtandao wa WhatsApp ili kuweza kupata kipengele hiki, ukiona unatumia toleo jipya kabisa na hujapata kipengele hiki huna budi kusubiri.
Ukiwa na kipengele hiki ukitaka kutuma meseji utakua unajiona mwenyewe pale juu kabisa katika sehemu ya mawasiliano katika mtandao huu.
Ukiingia sehemu yenye jina lako basi unaweza ukaanza kujitumia kila kitu ambacho unakitaka na itakua kama ni sehemu ya kuhifadhi vitu vyako au unaweza kusema ikawa sehemu ya kutunza kumbukumbu.
Kingine ni kwamba unaweza uka’pin jina lako juu kabisa ya mazungumzo yote ili kuhakikisha kuwa unapata kumbukumbu zako kwa urahisi kabisa.
Huduma hii kwa mitandao mingine sio jambo la kushangaza maana kuna baadhi ya mitandao ina huduma kama vile ‘Note to Self’.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani unaweza ukawa unatumia kipengele hiki katika mtandao wako wa WhatsApp?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.