Google ndio mtandao unatembelewa sana kwa siku, hili lipo wazi licha ya mtandao huo kuwa na sifa hiyo bado unafanya juu chini kuleta vipengele kadha wa kadha na kwa sasa wamekuja na kipengele kingine.
Kipengele ambacho kimeongezeka ni kwenye eneo la utafutaji pale – Google Search —kuwa na uwezo wa kuonyesha matafuto mengi tofauti na mara ya kwanza
Ni wazi kwa mara ya kwanza ilikua ukifika chini kabisa ilikua inakuladhimu kuingia katika ukurasa unaofuata kwa kugusa katika namba husika ya ukurasa mfano 2.3.4.5 n.k
Kwa sasa hili litakua haliwezekani tena na mtafutaji anaweza akashuka chini na kuona maonesho ya kurasa mpaka sita ndani ya onesho moja.
Jambo hili limewezeshwa katika komputa tuu lakini kwa upande wa simu unaweza ukashuka chini katika matafuto yako bila kufika mwisho.
Starting today, we’re bringing continuous scrolling to desktop in English in the U.S. so you can continue to see more search results easily. When you reach the bottom of a search results page, you'll now be able to see up to six pages of results. pic.twitter.com/xIuVP24FFm
— Google (@Google) December 5, 2022
Kingine ni kwamba kama mtandao huo wa Google ukileta matafuto hayo ya kurasa sita katika sehemu moja ukifika chini kabisa itakuambia angalia zaidi (See More).
Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana kwa watumiaji wa huduma hii kwa marekani tuu lakini sio muda mrefu kitaanza kupatikana kwa wateja wote.
Kipengele hiki hakina tofauti ukilinganisha na mitandao mingi ya kijamii ambapo unakua unashuka tuu mpaka ukifikie mwisho wa maudhui.
Kitu ambao Google imefanya mpaka kufikia uamuzi huu ni kwamba kwa tafiti ambazo wamezifanya wao wanasema kuwa hapo zamani watu waliotaka kuona majibu mengi ya matafuto waliingia mpaka kwenye ukurasa wan ne.
Hii inaonyesha dhahiri kuwa hakuna haja ya kuwa na namba ya kurasa nyingi wakati kuna hati hati kubwa sana kwamba watu wengi hawatafika katika kurasa za namba za juu.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unaona muonekano huu mpya utarahisisha chochote au bora tungebaki na ule wa zamani tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.