Google wapiga marufuku uwepo wa apps za kurekodi mazungumzo ya simu kuwepo kwenye soko lake maarufu la apps la Google Playstore kuanzia Mei mwaka huu.
Ifikapo tarehe 11 Mei, apps zote zenye uwezo wa kurekodi mazungumzo ya simu zitaondolewa kutoka kwenye soko hili maarufu la apps kwa watumiaji wa simu za Android.

Sababu:
- Kwa muda mrefu uwezo wa watu kurekodi mazungumzo ya simu umekuwa unaleta mjadala mkali kwa wadau mbalimbali – wengi wakiona si sawa kwani yule wa upande wa pili anakuwa hafahamu kama anarekodiwa na mwenzake. Hivyo kuwa ni jambo linalokiuka haki za ufaragha.
- Sheria tofauti tofauti katika majimbo ya Marekani na kwenye mataifa ya Ulaya. Google pia imebidi aweke teknolojia inayowezesha na kuondoa uwezo huo kulingana na alipo mtumiaji wa simu husika, ili kutokuvunja sheria tofauti tofauti katika mataifa tofauti. Mfano: Kuna majimbo au nchi unaweza kwenda uwezo huo wa kurekodi ukaonekana kwenye simu yako, ila ukienda katika nchi/jimbo ambalo linasheria kali dhidi ya uwezo wa kurekodi mazungumzo basi simu ya Android itaficha uwezo huo.
Wengi wanaamini hakutakuwa na madhara sana kwa ambao bado watahitaji apps za namna hiyo. Uhuru mkubwa wa mtu kuweza kupakua apps kutoka sehemu nyingine – nje ya Google Playstore bado unawapa watu uhuru wa kuzitafuta apps hizo.
Je una mtazamo gani juu ya uwezo wa kurekodi mazungumzo kwenye simu? Je unadhani ni huduma yenye umuhimu wowote kwa watumiaji wa kawaida?
Vyanzo: Arstechnica na Google
Naomba kuuliza, hivi hawa watu waodukua na ku huck account ya mtu na akawa anaitumia yeye je huwa wanatumia njia gani za kiteknolojia? Kwakuwa password, email, vyote zinakuwa siri ya mmiliki, naomba kufahamu tafadhari
Ahsante kwa swali zuri. Kuweza kufanya udukuzi inahitaji mtu awe na uwezo wa kutengeneza programu fulani ambayo ndio itaenda kuwa chombo cha kuweza kuingia kwenye akaunti ya mtu. Sasa ili kuzuia wadukuzi wasingie kwenye akaunti inashauriwa mtu atengeneze nenosiri ambalo si rahisi kuotea. Mfano unaweza ukatengenza nywila ya mchanganyiko wa herufi kubwa/ndogo, namba na alama mbalimbali lakini pia inashauriwa kuwa na tabia ya kubadili nenosiri angalau kila baada ya mezi mitatu.