fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Google Intaneti Teknolojia Uchina

Mpango wa Google kurejea Uchina

Mpango wa Google kurejea Uchina
Spread the love

Kwa muda tuu zimekuwepo habari zikihusisha mpango wa Google kutaka kurudi Uchina jambo amabalo limezua wasiwasi kwa wanasiasa nchini Marekani na kutaka kupewa maelezo ya kina.

Dunia nzima inafahamu ukiwa nchini Uchina huwezi kupata huduma ya Google na hii ni baada ya Google kuacha shughuli zake mwaka 2010 lakini huenda mambo yakarejea kama hapo awali.

SOMA PIA  Apple katika teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe

Wanasiasa takribani kuna na wa sita (16) kutoka vyama vya Republicans na Democrats wameiandikia barua Google wakiitaka kueleza kama wanayoyasikia yana ukweli wowote au la!

Kinachotia hofu zaidi ni kwamba Google wanatengeneza toleo la ambalo litazua tovuti zinazozunguzia demokrasia, dini, haki za binadamu na maandamano huko Uchina.

Mpango wa Google

Mpango wa Gogle kurudi Uchina unaweza ukawa ni mapema zaidi kuliko ilivytarajiwa.

Moja ya viongozi wa juu kutoka Google amedai kuwa hawana mpango wa kupeleka kitu kinachodaiwa nchini Uchina katika siku za usoni. Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wamediriki kuacha kazi kama ishara ya kutokubaliana na mpango huo.

SOMA PIA  Ndege Ndogo Yakamatwa Ikiwa Inasafirisha Bangi Gerezani

Baidu ndio mbadala wa Google nchini Uchina kwa sasa na iwapo kama kinachosemwa kikatimia basi wananchi nchini Uchina watakuwa kwenye kifungo cha aina yake.

Vyanzo: Engadget, Reuters

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania