Kipengele hiki kitaanza rasmi katika vifaa vya iPhone, iPad na hata Apple TV 4K mpya na kitakua kianahusisha kuimba kwa wasikilizaji au watumiaji wa Apple Music.
Apple Music ni huduma ya k’stream muziki kwa huduma ya kulipia kwa muda (kifurushi) kama vile Spotify n.k.
Karaoke ni uwezo wa kuimba kwa kufuatisha maneneo ya muziki yanayopita katika screen, sasa pata picha huduma hii kuanza kupatikana katika App ya Apple Music.
Kinachofanyika ni kwamba utakua una uwezo wa kufuatisha maneno –kwa kuyaona– ambayo yanaimbwa katika mziki husika. Vile vile kufutaisha huko kutakua kunaambatana dhahiri na muziki unavyokwenda.
Vile vile utakua na uwezo wa kuongeza sauti ya muziki na kupunguza kama ukitaka ujisikie vizuri namna unavyoimba.
Apple wanasema kuwa wanajikita katika kuhakikisha kuwa huduma hii inakwenda sawa kama wanavyotaka wao maana kuna hadi uwezo wa kuimba watu wawili.
Na bado hawataishia hapo katika kuhakikisha kuwa watazidi kuboresha huduma hii. Ni wazi kwamba kuna App nyingi ambazo zinatoa huduma hii lakini Apple bado hawajachelewa.
Moja katika huduma pendwa katika App ya Apple Music ni uwezo wake wa wimbo kuimba huku ukiwa unaonyesha maneno (mashairi) –yanayoimbwa— katika wimbo huo.
Kipengele hiki kinaitwa Apple Music Sing, Apple wanasema kuwa kipengele kitakuja muda fulani ndani ya mwezi huu na kitakua kinatumika katika vifaa vya Apple lakini kwa upande wa TV ni lazima uwe na toleo la Apple TV 4K.
Chanzo: TheVerge
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani unaweza ukawa unatumia kipengele hiki au ulikua unafurahia kuona tuu mashairi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.