fbpx
apps, Facebook, Intaneti

Facebook yaleta kitu kipya ndani ya app yao

facebook-yaleta-kitu-kipya-ndani-ya-app-yao
Sambaza

Facebook wanazidi kuboresha app yao na hasa hasa kuwapa watumiaji wake taarifa zaidi kuhusu vitu au kurasa/pages zinazoweka vitu vyake kwenye mtandao huo. Kwa sasa imekuwa rahisi mtumiaji kuona historia na taarifa zingine kuhusu ukurasa flani kwenye mtandao huo na pia kwa nini anaonesha post za page husika.

Meneja bidhaa bw Ramya Sethuraman, amezindua kitu kipya kitachopatikana ndani ya app ya Facebook kuanza sasa . Kitu hicho kilichoongezwa ndani ya app ya Facebook ni uwezo wa mtumiaji kuweza kufuatilia na kupanga vitu anavyotaka kuviona kutoka kwa marafiki zake, page na magroup aliyokuwapo ndani ya ukarasa wake wa Facebook, kwa kingereza kinaitwa “Why am I seeing this post “.

INAYOHUSIANA  Ujio wa toleo jipya la Fifa 17! #Gemu

Picha : Facebook

Mbali na hii pia facebook wameongeza kuimalisha kipengele cha zamani kinachofanana na  hicho, cha ” Why am I seeing this ads ” ambacho kilikuwa kinahusisha jinsi ya kuchagua matangazo ambayo mtumiaji anataka kuyaona na asiyopendelea kuyaona.

Picha : Facebook

lengo kubwa la features hizi ni mtumiaji wa facebook kuweza kuona post na matangazo anayoyapenda tu katika ukurasa wake na kuwafanya watumiaji kupenda zaidi app hii.

INAYOHUSIANA  Facebook kuja na sarafu yake ya kidijitali mwaka 2020

Je wewe kama mtumiaji wa facebook unapenda kuona vitu unavopendelea wewe katika ukurasa wako?

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Lymo

A Cyber Security Guy | A student | I Know A lot