fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook sms Teknolojia

Jibu Meseji Za Kawaida Na Zile Za Facebook Messenger Ukiwa Sehemu Moja! #Android

Jibu Meseji Za Kawaida Na Zile Za Facebook Messenger Ukiwa Sehemu Moja! #Android

Spread the love

Facebook Messenger katika mpango wake wa kuhakikisha kuwa inakuwa ndio namba moja kwa App za kutuma na kupokea meseji.

Imetoa kipengele ndani ya Facebook Messenger ambacho kitawezesha meseji za Facebook na meseji za kawaida katika simu yako kuonekana katika eneo moja. Hii inamaanisha mtu utakuwa na mamlaka ya kujibu meseji zote (aina mbili) ukiwa katika sehemu moja

facebook-messenger
Baadhi ya vipengele vya hali ya juu na vizuri sana kutoka katika Facebook Messenger havitaweza kutumika hapa – lakini huwezi jua labda maboresho zaidi yanakuja – lakini bado utakuwa na uwezo wa kutuma vitu jama vile zile stika

Facebook kwa upande wao wamesema kuwa watu wawe na amani na usalama wao kwani meseji za kawaida wanazotumiana wateja wao, kule wao hawazioni. Pia kingine ni kwamba watu wawe na amani tuu kwani kampuni haitaweza kupitia hata meseji zao za kawaida katika simu (kumbuka meseji za Fb na za kawaida zitakuwa katika sehemu moja)

Jambo hili lina faida kwani inamaanisha kuwa mtu hatakuwa na usumbufu wa kufungua na kufunga App ili mradi tuu aweze kujibe meseji zake za kawaida na zile za Facebook

Malipo yatakuwa ni kama kawaida yaani kwa zile Meseji za Facebook Messenger kama kawaida intaneti itahitajika wakati huku kwa SMS za kawaida viwango vyake vya uhataji vitatumika

Meseji Za Kawaida Zikiwa Na Rangi Ya Dhambarau Wakati Zile Za FB Zikiwa Na Rangi Ya Bluu

Ili kutofautisha kati ya zile za FB na zile za kawaida itakuwa hivi; zile za Facebook zitakuwa ni za bluu wakati hizi za kawaida zitakuwa ni za rangi ya zambarau

SOMA PIA  Kompyuta/Tabiti isiyochosha kuibeba

Huduma hii kwa sasa inapatikana tuu kwa wale wanaotumia vifaa vyenye programu endeshaji ya Android tuu

Mtumiaji atakuwa na uwezo wa kuchagua kama aifanye Messenger kuwa sehemu yake ya siku zote (default SMS App) ya kupitia meseji zake zote (facebook na kawaida) au la

SOMA PIA  Programu tumishi 46 zaondolewa kwenye Google Playstore

Facebook kama kawaida yao huwa hawalali, mara kwa mara huwa wanajaribu kugundua vitu na njia mbalimbali ambazo zinaweza zikawafanya watumiaji wa huduma zao kufurahia huduma hizo.

Hili swala zima la kuweza kukusanya meseji zote katika sehemu moja halijaanza leo, mwaka 2012 kampuni lilifanya hivyo lakini ndani ya mwaka huo huo kipengele hichi kiliondolewa kutokana na kwamba kulikua na watumiaji wachache

Sasa wameamka tena, je wewe unaona muda huu watafanikiwa juu ya kipengele hiki? Tuandikie hapo chini sehemu ya comment.

Tembelea mtandao wako pendwa kila siku ili kujipatia habari mbalimbali zinazohusu teknolojia kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania