fbpx
Anga, Teknolojia, Uber, Usafiri

Huduma za usafiri wa kukodi njia ya anga

huduma-za-usafiri-wa-kukodi-njia-ya-anga
Sambaza

Mamlaka ya safari za anga nchini Australia, CASA imefahamisha kuwa mradi wake wa huduma ya usafiri wa kukodi njia ya anga unakaribia kukamilika.

Katika safiri huo wa kukodi kwa njia ya anga yapo makampuni mbalimbali yameshajitokeza kutaka kuwekeza nchini humo na mojapawapo ikiwa Uber ambao tayari walishakaa meza moja na wahusika kujadili suala hilo.

Usafiri huo ni sawa na kukodi helikopta isipokuwa tu wenyewe utakuwa ni wa gharama nafuu zaidi. Mbali na hapo watakuwa wanatumia njia maalum ambazo zitakuwa zinaongozwa na taa za barabarani.

Huduma za usafiri wa kukodi
Usafiri wa anga kwa kukodi unatazamiwa kukamilika ndani ya miaka mitao ijayo huko Australia.

Mbali na Uber kutarajia kuwa mmoja wa watoa huduma hiyo ndani ya miaka mitano ijayo lakini wanatazamiwa kutoa huduma kama hiyo nchini Marekani mwaka 2020.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  WhatsApp yaboreshwa: Sasa Mazungumzo yako Yapo Salama Zaidi
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.