Hivi unakumbuka kale kahali unakujisikia punde tuu ukijua kama ‘Wallet’ yako imeibwa au umeisahau mahali? Mimi ninakakumbuka aisee
‘Wallet’ ni kitu cha muhimu sana na kumbuka sio tuu utakuwa umepoteza pesa zako bali na vitu vya muhimu kama vile kadi za benki na vitambulisho vingi vya muhimu n.k.
Kwa sasa Wallet iliyopewa kwa jina la ‘The Ekster 2.0” ipo sokoni na lengo kuu ni kuja kukuokoa juu ya swala zima la kupoteza/kusahau wallet. Hebu jiulize ni mara ngapi umeisahau na ukashindwa kukumbuka pale ulipoicha?
Kingine kizuri kuhusiana na ‘Wallet’ hii ni kwamba inaweza ikapatikana kwa kutumia msaada wa teknolojia ya kujua mahali ilipo (location)
Kumbuka hii sio Wallet janja ya kwanza kuja katika soko hata mwaka 2015 ‘Woolet’ iliingia sokoni kama Wallet janja pia. Kitu ambacho ‘Ekster’ imeizidi ‘Woolet’ ni kwamba yenyewe inaweza ikamsaidia mtu kuweza kujua ni eneo lipi ambalo amaesahau ‘wallet’ yake wakati ‘Woolet’ ilikuwa inaweza kumpatia taarifa tuu kama ‘Wallet’ imeibwa au imepotea
VITU VYA NDANI
‘Wallet’ hii ni ya kwanza kabisa kutumia nishati ya umeme. ‘Wallet’ hii inahitaji ujazo wa juu wa nishati wa Lux 800 ili kujaa chaji kabisa. Na hii inapelekea kutokuwa na ulazima sana wa kuichaji katika jua kali, mwanga wa kawaida tuu unatosha.
Wallet hii ita ‘Sync’ na simu janja kwa kutumia huduma ya ‘Bluetooth’. Na pia kwa msaada wa App ya Tile basi mtu anaweza akapewa taarifa za mahali ambapo Wallet yake ilioneka kwa mara ya mwisho.
‘Tile’ ndio mtandao mkubwa sana wa kujihusisha na Upoteaji na upatikanaji wa vitu. Yaani mtumiaji atapata ‘Notification’ ya mahali pa mwisho pa Wallet hiyo kuonekana katika simu yake na hata pale mtumiaji mwingine wa ‘Tile’ atakapopita karibia na ‘Wallet hiyo (Ekster) iliyopotea au kuibwa
BEI
Kwa kuwa ‘Wallet’ hii iko ya aina mbili moja kwa jina la ‘Parliament’ (Ambayo ina vyumba 10 vya kuhifadhia kadi) inauzwa dola 99 za kimarekani ambazo kwa haraka haraka ni sawa na 215,000.
Aina nyingine ni ‘Senate’ ambayo ina vyumba 7 vya kuhifadhia kadi na pia uwezo wake wa ‘Tracker’ ni mdogo ukilinganisha na Parliament. Hii inauzwa dola 79 za kimarekani ambazo kwa haraka haraka ni sawa na shilingi 172,000.
Bei hizi zote mbili zinajumuisha na gharama ya ‘Tracker’ lakini kama mtu hutaki kununa na ‘Tracker’ zake basi unaweza ukapata bei ambayo iko chini ya hapo
‘Wallet’ hizi kwa sasa zinapatikana katika soko la mtandao tuu, hivyo kama mtu anazihitaji basi hana budi kuzitafuta katika masoko hayo
TAZAMA
Je wewe ni mmoja kati ya wale wanaosahau au kupoteza ‘Wallet’ zao mara kwa mara? Niandikie hapo chini sehemu ya comment unahisi hii itakusaidia vipi?