Mozilla ni kampuni isiyo ya kibiashara ambayo ina mchango mkubwa sana japokuwa watu wengi hawalijui hili.
Mozilla — samahani, namaanisha Moz://a — inatoa huduma ya ‘open web’ hii inamaanisha kuwa bidhaa zake nyingi zinapatika bure katika mtandao.

Mozilla ndio kampuni ambayo inamiliki kivinjari cha Firefox, maarufu kama Mozilla Firefox. Licha ya kuwa kivinjari hicho hakifanyi vizuri sana siku hizi kulingana na mapinduzi ya nguvu yaliwekwa na vivinjari vya Chrome, Edge na vinginevyo.
Ukiachana na hayo kampuni imetangaza mabadliko makubwa na hii ikiwa ni sambamba na kubadiilisha logo yake.
Katika logo mpya alama kama vile :// zimeonekana ambazo pia huwa zinaonekana kwenye vivinjari katika eneo la kuandika tovuti.
Mozilla walidai kuwa rangi zao wamezipata kutoka katika Firefox na vivinjari vingine na pia rangi ya logo mpya ya Mozilla itabadilika kulingana na sehemu au mazingira ambayo logo hiyo itatumika. kwa kulielewa hili zaidi tazama picha hapo chini

Kingine ni kwamba font (maandishi ya kifaa cha kielektroniki) ambazo zimetumika katika kutengeneza logo hiyo mpya zinaitwa Zilla ambazo pia zinapatikana bure katika mtandao hivyo mtu yeyote anaweza kuzishusha na kuanza kuzitumia kama font zingine tuu.

Ukiachana na kubadilisha logo yake labda kuna jambo lingine kubwa linakuja kwani Mozilla kwa kipindi cha muda mrefu imekua kimpya sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako je wewe unalichukuliaje jambo hili na ukiangalia Mozilla ni kampuni ambayo haijajikita katika kutengeneza faida juu ya bidhaa zake, bali huwa mara nyingi inazitoa bure katika mtandao. Niandikie hapo chini sehemu ya comment.
Chanzo: Blog Ya Mozilla
One Comment
Comments are closed.