fbpx
Teknolojia

Uwezo wa kuzuia makelele kwenye Zoom Meeting

uwezo-wa-kuzuia-makelele-kwenye-zoom-meeting
Sambaza

Katika ulimwengu wa sasa na hasa wakati huu ambapo Dunia inapambamba na janga la virusi vya Corona mambo mengi tuu yameweza kuamuamuliwa kwa njia ya Zoom Meeting inayohusisha mawasilano katika mfumo wa maandishi bila kusahau picha jongefu.

Mimi ni kati ya wale ambao naamini katika matumizi ya teknolojia katika kufanikisha jambo fulani bila ya watu kuonana ana kwa ana ili kuweza kufanya mazungumzo, kutoa maamuzi, n.k hivyo kutumia vitu kama Google Meeting, Skype, Zoom kufanya mikutano huku kila mhusika akiwa sehemu yoyote duniani.

Si mara moja au mbili tumeweza kusoma habari mbalimbali zinazohusu Skype, Zoom Meeting kufanyiwa maboresho mbalimbali kufanya programu hizo kukidhi mahitaji ya watu wanaozitumia. Safarii hii kwenye Zoom toleo la 5.2 kuna mapya yafuatayo:-

 • Uwezo wa kuzuia makelele ya nje. Inalazimu wanaokutana kupitia Zoom kuzima kipaza sauti cha kwenye kifaa husika ili kutoleta bu mkanganyiko wa kusikia ambayo hayawahusu wengine. Katika kipengele kipya mtu ataweza kuweka mpangilio wa kufanya makele ya nje kutosikika bila ya kufunga kipaza sauti. Kuruhusu kipengele hicho ingia “Video Settings > Audio > Suppress background noise” na mtu ataweza kuamua kufanya mengineyo (ya nje) yasikike kwa kiwango gani.

  kuzuia makelele
  Uwezo wa kuzuia makelele ya nje kwenye Zoom Meeting toleo namba 5.2.
 • Kuongeza nakshi nakshi wakati wa kuonyesha washiriki kile ulichokiandaa kwa ajili yao (kwa Kiingereza: Overlay video presentations),
 • Picha ya mshiriki kuonekana imerembwa. Inawezekana kabisa muda wa kuingia kwenye mazungumzo umewadia ukiwa sehemu  ambayo usingependa waone uhalisia wa kile ambacho kipo nyuma ya mahali husika na,

  kuzuia makelele
  Kuweka kitu tofauti nyuma kuficha uhalisia wa mahali husika.
 • Uwezo wa kuamua namna gani picha yako ionekane wakati wa mazungumzo. Katika hili mtu ataweza kuongeza/kupunguza ukubwa wa muonekano wa sura/picha mnatokulingana na itakavyofaa. Kip[engele hicho kwenye Zoom kinaitwa “Touch up my appearance” ndani ya mpangilio wa picha mnato.

  kuzuia makelele
  Sasa unaweza ukaamua namna gani picha yako ionekane wakati wa kufanya mazungumzo ndani ya Zoom Meeting.
 • Kuonyesha hisia kwa kutumia vikatuni mbalimbali. Kwenye toleo hilo jipya vimeongezwa vikatuni mbalimbali ambapo mtu anaweza kuvitumia kuonyesha ishara ya kukubaliana na jambo, kucheka, huzuni, n.k.

Hayo ndio mapya yanayopatikana ndani ya Zoom Meeting toleo namba 5.2. Ni wewe tuu kupakua toleo hilo jipya kulingana na kifaa ulichonacho. Endelea kutembelea tovuti yetu kila leo kupata habari zinazohusu masuala ya teknolojia.

Chanzo: Gadgets 360

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Gari la Mitsubishi Outlander linaweza kudukuliwa kwa njia ya WiFi
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|