fbpx
Mtandao, Teknolojia

Drones kuboresha 4G katika mikusanyiko ya watu! #Teknolojia

drones-kuboresha-4g-katika-mikusanyiko-ya-watu
Sambaza

Kampuni ya mawasiliano ya marekani ya AT&T imeanza mpango wa kutumia Drones katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu wengi kama vile maeneo ya matamasha ili kuboresha intaneti ya 4G.

drones
Picha kwa hisani ya mtandao

AT&T wanafanya hivi ili kukabiliana na hali ya minara kuzidiwa na watumiaji hasa wakati wa mikusanyiko, kama ulishawahi kuhudhuria tamasha la nyamachoma Dar es salaam kwa mfano utakuwa umekwisha kutana na hali hiyo. Minara inapokuwa imezidiwa na wingi wa watu wanaotaka kutumia huduma za mitandao kwa wakati mmoja hushindwa kufanya kazi katika ubora hii hupelekea mawasiliano kuwa magumu.

INAYOHUSIANA  IJUE “SOLAR IMPULSE 2″ NDEGE INAYOTUMIA UMEME JUA

Tokea teknolojia ya Drones ilipoingia sekta nyingi zimenufaika na teknolojia hii, tumeona mapinduzi katika utengenezaji wa video za miziki hapa bongo baada ya drones kutumika pia tumeona ukusanyaji wa taarifa za kitafiti pia kumepata mabadiliko baada ya drones kuanza kutumika katika tafiti mbalimbali.

Kimsingi ujio wa Drones umegusa sekta nyingi za aina mbalimbali, pia yapo mambo mengi ambayo utendaji kazi wake umebadilika katika sekta ya mawasiliano baada ya drones kuanza kutumika

AT&T wanataka kurusha drones ambazo zitakuwa kama minara midogo ambayo itaisaidia minara mikubwa katika maeneo ambayo kuna mikusanyiko ambayo siyo ya kudumu.

INAYOHUSIANA  Lenovo yazindua kompyuta mbalimbali katika maonyesho ya E3 2018
MWC-drones-2-5-1080x675
Drone. Picha kwa hisani ya mtandao

Huduma kama hizi zitatumika wapi?

Huduma hii haitakuwa na manufaa katika maeneo ya matamasha na starehe tu ila hata wakati wa majanga mbalimbali ambapo watu wengi hujaribu kuwasiliana kwa wakati mmoja, wakati wa mabomu ya Gongo la mboto kwa mfano kuliibuka taflani na kwa sababu watu wote walijaribu kuwasiliana na ndugu zao kwa simu jambo lililosababisha minara kuzidiwa na kushindwa kazi, nyakati kama hizi kampuni za simu zinaweza kutumia minara iliyofungwa katika Drones kuweza kutoa huduma za simu.

Kama njia hii inayojaribiwa na AT&T itafanikiwa basi tutegemee mabadiliko haya kufika pia huku kwetu na pia tutegemee kuona makampuni ya simu yakishindana kutoa huduma za intaneti katika mikusanyiko mbalimbali

INAYOHUSIANA  Programu tumishi inayoweza kutambua kuzidi kiwango cha dawa yaundwa

Je kwa sasa Drone zinatumika wapi hasa?

Kwa sasa teknolojia ya drone inatumiwa na makampuni ya simu kwaajiri ya kuikagua minara yake ya simu kwa kuwa gharama ni naafuu kulinganisha na binadamu anapofanya kazi hii lakini pia kunasehemu za minara binadamu asingeweza kufikia kuzikagua.

Teknolojia hii bado haijaanza kufanyiwa kazi ila ipo katika majaribio an makampuni mbalimbali yanaifanyia majaribio ikiwamo Google.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Nickson