Mgombea wa uraisi marekani Hillary Clinton amekamata fursa ya Pokémon Go baada ya kuanzisha kampeni ya kuwaandikisha na kuwaelimisha wapigakura juu yake katika vituo maalumu vya gemu hilo.

Timu ya kampeni ya Clinton imeonekana kutaka kuandikisha na kuelimisha watu wengi hasa vijana juu ya mgombea wa uraisi wa Marekani Hillary Clinton kwa kuandaa vituo katika maeneo mbalimbali ambayo pia yanatumiwa na Pokémon Go kama maeneo ya mazoezi (gym) na Pokéstop.
Pokémon Go ni nini?!
Pokémon Go ni gemu ambalo wachezaji wanatakiwa kutembea katika mitaaa (inakubidi kutembea mitaani kucheza gemu hii) wakiwinda wanyama wadogo ambao wanaitwa Pokémon na pindi mchezaji anapomuona mnyama basi hutumia mipira kupiga na kuwakamata wanyama hao.
Soma Zaidi: Pokemon Go: Gemu Tishio kwa mitandao ya kijamii
Katika gemu hili pointi inapatikana kadiri unavyokusanya wanyama lakini pia kwa kupigana na wachezaji wenzako, ili kupigana na wachezaji wengine basi inabidi kwenda katika Gym ambazo ni sehemu maalumu kwamfano hapa Dar es salaam Posta ya zamani katika bustani ya NBC kuna gym ambayo unaweza kupigana ili kuongeza pointi zako.

Kwa mujibu wa mtandao wa Vox timu hiyo ya kampeni ya Clintoni imeamua kuandikisha wapiga kura katika vituo viwanja na bustani ambazo wachezaji wa gemu hili wanaenda kuongeza pointi za mchezo, hii fursa ya kipekee kuwapata vijana wengi kujiandikisha kupiga kura na pia kuweza kumnadi mgombea huyo anayewania tiketi ya kukiwakilisha chama chake.
Je makampuni ya uandaaji wa matamasha na promosheni yajifunze nini?!
Yapo mambo mengi ambayo makampuni ya promosheni na waandaaji wa matamasha wa hapa nyumbani wanaweza kujifunza kutoka kwa timu ya kampeni ya Clintoni. Huu ni mfano tu wa namna ambavyo gemu hii inaweza kutumiwa na makampuni mbalimbali kuweza kuwavuitia wateja kuja katika biashara zao.
Mashirika ya Umma, makampuni na kampeni za kijamii za nchini wanatakiwa kuhusisha masuala ya teknolojia za kisasa kama vile mitandao ya kijamii na kuiangalia kama nafasi ya kuwafikia watu na badala ya kuwa na jicho la kuitazama kwa hasara zake badala ya fursa inayopatikana ya kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi.
One Comment
Comments are closed.