fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

simu Smartphones Xiaomi

FUNUNU: Tutegemee Simu Janja Zenye ‘Display’ Nyuma Na Mbele!

FUNUNU: Tutegemee Simu Janja Zenye ‘Display’ Nyuma Na Mbele!

tecno

Kwa sasa zile ambazo tunaziona au tuliziona kama ni za ajabu kabisa ni zile simu janja za kukunja (foldable phones), hizi ambazo zitakuja na ‘display’ mpapa kwenye eneo la nyuma la simu janja zinaweza kutuacha midomo wazi pia.

Teknolojia inakua kwa kasi sana, teknolojia ya simu ni wazi imekua kwa kasi mpaka hapa tulipofikia na kama kawaida huwa teknolojia hizi zinavyokua basi huwa zinaua matumiza ya vifaa vingine ambavyo vilikua vinajitegemea kwa mfano, tochi, mp3 na ipod na vingine vyote

SOMA PIA  Sasa Badilisha Maelezo ya Picha katika Instagram

Ni wazi kuwa ukiwa na simu janja unaweza maliza mambo mengi sana tofauti ukiwa na simu ambayo sio janja…. baada ya kujua kuwa teknolojia ya simu inabadilika sana.. sasa ni kitu gani kitakuwa ni kipya ambacho matoleo mapya ya simu yatakuja nacho?

tecno

Digital Chat Station Waliandika Hivyo

Digital Chat Station Waliandika Hivyo

Swali ni gumu sio? ila vyanzo vingi vinasema kuwa watu wakae tayari na kutegemea simu ambazo zitakuwa hazikunjiki na pia zitakuwa na ‘display’ katika eneo lake la nyuma!

SOMA PIA  Airtel Yashika Nafasi ya Nne Duniani!

Kutokana na fununu hizo inasemekana kuwa mwaka huu Xiaomi Mi 11 Ultra kutoka Xiaomi ndio itakua simu inayokuja na aina hiyo ya ‘display’ .

Ukiachana na hili ni kwamba mpaka picha zikionyesha muundu wa ‘display’ hiyo ya nyuma zimesambaa katika mitandao mbali mbali.

Inayosemekana Kuwa Xiaomi M11 Ultra

Inayosemekana Kuwa Xiaomi M11 Ultra

Ukiachana na Xiaomi makampuni kama Huawei nao walijaribu kusema kuwa watakuja na teknolojia hii katika simu kwa mwaka jana ila hatukuona hilo likifanyika! je na Xiaomi watakuwa ni hivi hivi? la msingi ni kwamba inabidi tusubiri.

SOMA PIA  Matangazo Ya Samsung Kuwa Vifaa Vya Kuchajia Galaxy S10!

Ningependa kusikia kutoka kwako, Unadhani simu ya aina hii ikitoka italeta chachu yeyote na kufanya watu walifikirie soko la simu janja kivingine tofauti na mwanzo?

Kwa watengenezaji wa simu pia hali unadhani itakuwaje? niandikie hapo chini katika sanduku la maoni, Pia usisahau kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo nawe katika teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania