Akiwa kama mtengenezaji mkubwa wa vifaa vya elektroniki, kampuni ya Samsung imeendelea kupanua shughuli zake za viwanda ulimwenguni kote.
Samsung wametangaza kufungua milango ya maendeleo katika mji wa Noida nchini India kwa kufungua kiwanda kikubwa cha kutengeneza wa simu. Hata hivyo, wana viwanda nchini za Marekani, Brazil na Korea Kusini kama makao makuu. Kukua kwa ufanisi wa simu za Samsung kupelekea kampuni hiyo kuwekeza kwa kufungua kiwanda katika nchini India.
Kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha simu milioni 120 kwa mwaka. Mbali na simu pia watakuwa wanatengeneza TV na majokofu. Eneo ambalo kiwanda hicho kitajengwa lina ukubwa wa ekari 35.
Takwimu zinaonyesha asilimia 10 ya simu zinazozalishwa na Samsung zinanunuliwa katika soko la India.