Hapo mwanzo kulikua kuna viashiria vingi ambavyo vilikua vinaonyesha moja kwa moja kwamba toleo la iPhone 15 halitauzika sana nchini China.
Ni wazi kwamba nchini China Huawei imetoa simu janja yake mpya ambayo imeleta mapinduzi na ukiachilia hayo bado serikali ya nchini humo iliwekea vikwazo kwa kwa ujamla hata hizi iPhone 15!
Na kikwazo hicho ni kwamba ilikataza kwa watumishi wote wa serikali kutotumia simu za iPhone, hii ikiwa ni moja ya njama ya kuhakikisha kuwa wanatumia vitu vyao na hata kuhimiza wananchi wake kufanya hivyo.
Hali hizo zote mbili zilipelekea watu kudhania kuwa Apple wakitoea toleo la iPhone 15 basi watapata shida sana katika kuuza kwenye soko hilo.
Hali imekua ni tofauti sana maana mara tuu baada ya matoleo hayo kutangazwa rasmi mtandao wa Apple wa huko China ulipitia wakati mgumu (tatizo la kiufundi) baada ya kupata idadi kubwa ya watu wanaoingia katika tovuti hiyo.
Licha yah ivyo hata vyanzo vingine vya mauzo ya simu hiyo na venyewe vilishambuliwa kwa kiasi kikubwa mfano wale ambao huwa wanauza kabla simu hazijafika (Pre-orders) na wenywe walipokea namba kubwa ya watu wenye uhitaji.
Masoko yanayomilikiwa na Alibaba kama vile Tmall na JD.com pia yamekua yakipata namba kubwa ya wateja wa oda za mwanzo nyingi.
Napenda kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je kwa hayo yote yaliyototkea ulikua unadhani kwamba iPhone 15 itapata mapokezi haya?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.