fbpx
Blackberry, Samsung, Teknolojia

BlackBerry Wajiunga Na Samsung Katika Kutengeneza Tablet Ya Ulinzi/Usalama Wa Hali Ya Juu!

blackberry-wajiunga-na-samsung-katika-kutengeneza-tablet-ya-ulinziusalama-wa-hali-ya-juu
Sambaza

Kitu cha kusikitisha ni kwamba hutaweza kuimiliki Tableti hii kwani inatengenzwa spesheli kwa ajili ya serikali ya ujerumani.

Hilo likiwa kichwani, kama inavyojulikana kuhusu kampuni ya Blackberry. Kampuni hiyo ina sifa kubwa ya kuweka usalama na ulinzi mbele ukiachana na mambo mengine yote. Kwa sasa kampuni inajiunga na kampuni ingine ambayo ina jina kubwa kabisa katika soko la simu duniani, Samsung.


Kampuni (ya Blackberry) lilitoa tamko hilo katika mkutano wa IFA 2016 ambao ulifanyika Berlin. Kampuni lilisema kuwa dhumuni kubwa la kuwa na wenzao wa Samsung katika kazi hiyo moja ni kuhakikisha kuwa wanazalisha Tableti ambayo itakuwa haiwezi kuchunguliwa (kudukuliwa) na hii itakuwa ni spesheli kwa ajili ya serikali y ujerumani.

INAYOHUSIANA  Kompyuta: Ubora uleule lakini faili ni dogo

Tablet hiyo itakuja na kitu kinachoitwa ‘Mobile Application Manager (MAM)’, teknolojia hii ina kazi kubwa sana na husaidia pale mtu anapotaka kubadilisha na kutumia Apps za binafsi au hata zile za ofisi katika kifaa kimoja. Hili linafayika huku mtu huyu akiwa bado ana uhakika kuwa kifaa chake kina usalama wa hali ya juu.

Kwa upande wa Samsung, wenyewe wataleta KNOX mezani wakati wenzao Blackberry wakihakikisha kuna usalama na ulinzi wa hali ya juu.

INAYOHUSIANA  Instagram wachukua hatua kupunguza Udukuzi

csm_SecuTABLET02_Homesecreen_f8490bf408
Wakati tunasubiria serikali ya ujerumani ipatiwe Tableti hiyo, kampuni ya Blackberry bado inajipa sifa na kusema kuwa imeshatoa huduma za kiulinzi na kiusalama kwa serikali zaidi ya 20 duniani kote.

Niandikie hapo chini sehemu ya comment wewe unaonaje jambo hili? Makampuni mawili yenye ushindani mkubwa lakini yameamua kukutana na kutengeneza kitu bora zaidi. Ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari na muajanja mbalimbali yanayohusu teknolojia kwa lugha ya Kiswahili. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com