Facebook wapata janga katika juhudi zao za kusambaza intaneti baada ya satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya intaneti yenye kasi barani Afrika kuharibiwa.
Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.
Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.
Satelaiti ya Amos-6 inakadiriwa kuwa na thamani ya $200m|Tsh bil. 440 na ilimilikiwa na kampuni kwa jina ‘Spacecom’.
Hakuna aliyejeruhiwa katika mlipuko huo. Facebook wanasema kuwa wataendea kujitolea wakiwa na lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na kufanya bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii.
Vyanzo: BBC, Space news