Tulishaandika kuhusu ujio wa simu ya BlackBerry inayotumia toleo la Android na sasa picha ramsi za simu hii zimevuja mitandaoni. Kwa sasa ni jambo la uhakika kabisa ya kuwa kuna simu BlackBerry inayotumia Android itaingia sokoni hivi karibuni.
Kwa haraka kulingana na picha hiyo, BlackBerry Venice ni simu inayovutia sana, na wakifanikiwa kuifanyia kampeni nzuri ya kimauzo watakapoileta sokoni rasmi basi ni jambo la bila ubishi ya kwamba simu hii itafanya vizuri sokoni.
Sifa zake;
- Uwepo wa keyboard kwa ajili ya kuandika, pia itakuwa na uwezo wa mguso (touch screen).
- Kamera ya MP 18
- Vingine vingi vitambulika baada ya utambulisho rasmi kufanyika
Kwa sasa muonekano wake ni wa kuvutia na hakuna ubishi ata itakapoingia sokoni haitakuwa simu ya bei rahisi.
Tunaamini ili ni toleo la mwanzo tu kwa ajili ya watu wachache wanaohusika katika matengenezo ya simu hiyo na hivyo bado kuna mambo yanayoweza kubadilishwa hadi kufikia hapo watakapoitambulisha simu hii rasmi.
Je wewe umekuwa mpenzi wa simu za BlackBerry? Je unadhani uamuzi wa kutengeneza simu zinazotumia Android ni uamuzi bomba? Tuambie
No Comment! Be the first one.