Mpenzi Android,
Ni miaka tisa tayari. Inaonekana kama jana tukiazimisha mazazi ya Froyo. Lakini sasa tupo na kichanga chetu Oreo.
Baada ya miaka yote hiyo, Android kamwe hujaonekana kama ni bora. Vingi vimebadilika tangu siku ya kwanza tulipokutana.
Ndio, bado nakumbuka Mpenzi Android. Nilikuwa katika duka la simu mwaka 2008, wakati nakatiza ndipo nilipokuona. T-mobile G1. Ulikuwa ndani yake.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wetu. Umekuwa sana mpenzi, pamoja na kwamba ulionekana kama unayejitolea na hukuwa na dhamana ya kueleweka.
Nilidhani mambo hayawezi kuwa mazuri. Lakini ulitambulisha ujio wako kwa mambo kadhaa mazuri na mengi. Tuliyachukulia mambo kwa utaratibu na upole. Nilijua hatukuwa peke yetu na tuliwaona wengine wakifanya kama sisi.
Lakini pindi ulipoweka Nexus mkononi mwangu, kila kitu kilibadilika. Uliwavutia wengi na nilijua sasa tupo pamoja zaidi ya wakati wote.
Hakuna mahusiano yaliyo kamili. Najua unachukia hali zangu za kiuchumi, madai yangu kuongeza uhai wa Betri zetu na udogo wa kioo chako. Na hakika umebadilika na kudhibiti mipaka yako ya usalama. Ila ntamisi sana uhuru uliokuwepo awali
Tumeongezeka mno na mambo yamebadilika. Wakati mwingine ninahisi kama tunahitaji tu kuwasiliana zaidi.
Tulizoea kutumia Hangout, lakini sasa tunatumia Allo, japo tulijaribu kutumia Duo mara moja moja. Lakini tulijaribu mpenzi.
Pamoja na miaka yote tisa lakini bado tuna nguvu. Na sasa tunatarajia mapacha wetu Pixels ambao wapo njiani kuzaliwa mwaka huu.
Nadhani nimejaribu kusema kitu Mpenzi Android.
Happy Anniversary.
NB:
Android kwa mara ya kwanza ilianza kutumika tarehe 23, mwezi Septemba 2008.
Froyo (Verion 2.2) ni toleo mojawapo la Android. Oreo (Version 8) ni toleo la sasa la Android. Pixel: mwaka huu Google wanatarajia kutoa simu mbili za Pixel. Google Allo ni programu ya kuchati kama WhatsApp. Google Duo ni programu ya kuchati kwa njia ya video. Hangout pia ni programu ya kuchati pia.