Instagram wamekuja na app mpya inayojitegemea inayoitwa Layout. App hii utakayoweza kuitumia ata kama hauna akaunti Instagram itakuwezesha kuweka picha katika makundi kutengeneza picha moja. Na pia itakuruhusu kufanya mengi kama kuchanganya picha mbili kutengeneza moja.
Kwa kiasi kikubwa tayari kuna apps nyingi ambazo zipo zinazofanya mengi ambayo yanawezekana katika app hii ila ukweli utabakia kuwa Instagram wapo vizuri zaidi katika masuala ya picha, na hivyo ubora wa app hii ni wa juu sana. Ukiingia kwenye Google Play au App Store na kuandika ‘Collage’ na kutafuta utakutana na lundo la apps za kuchanganya picha ila wengi wana uhakika app hii kutoka Instagram itafanikiwa kutokana na Instagram kuwa tayari na jina kubwa kama tulivyoandika hapo juu.
Je utaipata lini?
App hii tayari inapatikana katika soko la App Store kwa ajili ya simu za iPhone na tableti za iPad ila bado haipatikani kwa ajili ya programu endeshaji ya Android. Instagram wamesema app hiyo itakuja kwenye soko la apps la Android miezi michache ijayo, lakini tayari Instagram walitoa ahadi hiyo walipokuja na app ya Hyperlapse (Bofya kuifahamu – Instagram Wakuletea App Mpya – Hyperlapse ) mwaka jana mwezi wa nane na app hiyo bado haipatikani kwa watumiaji wa Android, imebaki kwa iOS tuu.
Kupakua Layout kwenye iOS -> Layout (App Store)
No Comment! Be the first one.