fbpx

WhatsApp: Utaweza kufuta ujumbe ulioutuma kimakosa hata baada ya saa moja kupita

0

Sambaza

WhatsApp kuongeza muda wa kufuta ujumbe uliotumwa kimakosa, hii ni kutoka dakika moja ya sasa hivi hadi dakika 68 na sekunde 16.

Kwa muda mrefu sasa watumiaji wa app hii maarufu wamekuwa na uwezo wa kufuta ujumbe walioutuma kimakosa kwa wengine ndani ya sekunde 7 baada ya kuutuma – na wakishafuta ujumbe huo eneo linakuwa linabakia kuandikwa ‘this was deleted’.

Kupitia tovuti inayofuatilia matoleo ya apps katika kiwango cha majaribio, yaani BETA, wamegundua toleo lijalo la WhatsApp la Android limeruhusu watumiaji wa app hiyo kufuta ujumbe uliotumwa hata sekunde 4096 zilizopita – zinazofanya saa 1 dakika 8 na sekunde 16.

Kufuta ujumbe uliotuma kimakosa WhatsApp ata Lisaa 1 Baadae

Kufuta ujumbe uliotuma kimakosa WhatsApp

NJIA YA KUFUTA MESEJI ULIYOITUMA WHATSAPP – TEKNOKONA/WHATSAPP KUFUTA UJUMBE

Kwa wale waliokuwa wanatumia matoleo yasiyo rasmi ya WhatsApp ili kuwa na uwezo wa kufuta hadi ujumbe wa miaka 3 nyuma hilo halitafanikiwa tena, timu ya WhatsApp wamefanikiwa kuzuia hilo kufanyika kabisa.

INAYOHUSIANA  Kutopatikana kwa Google Allo

Je, wewe una mtazamo gani juu ya nyongeza hii ya muda? Je, tangu uwezo wa kufuta ujumbe uliotuma kimakosa WhatsApp kuja mwezi wa Oktoba mwaka jana umenufaika nao?

Chanzo: CNET

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.