Kampuni ya Apple inaingia katika ulimwengu Tamthilia (TV series). Mara hii itakuja na mchezo wa kuigiza (series) ambao unaitwa “Vital Signs” ambapo muhusika wake mkuu atakuwa ni Dr.Dre
‘Series’ hii itakuwa imeandaliwa rasmi na kampuni ya Apple (Apple Inaimiliki). Taarifa hii imepokelewa kwa namna tofauti tofauti na wengine hawakutegemea kabisa na wengine walitegemea kampuni ya Apple itafanya kitu hiki mwaka jana (2015)
Kwa upande mwingine mtu unaweza sema kuwa Apple inafuata nyayo za Amazon na Netflix. Makampuni hayo mawili yamepata umaarufu na pesa nyingi kupitia michezo yake ya kuigiza, “Transparent” kutoka Amazon na “Narcos” kotoka Netflix.
Kwa upande mwingine mtu unaweza ukasema kuwa video ya ‘Straight Outta Compton’ ndio inayoeleza chimbuko na maisha kamili ya msanii Dr. Dre. Na pia ni ‘Movie’ ambayo imefanya vizuri sana na kuweka baadhi ya rekodi. Hata hivyo bado kampuni linaweka hela yake ili kazi hiyo (series) ikamilike ili watu waone stori ya aina yake ambayo msanii huyo anataka kuwapatia watu
Mchezo huu wa kuigiza utakua ukionyesha sehemu ndogo ya maisha ya Dr. Dre ambayo ni ya ukweli kabisa na sehemu nyingine ikiwa ni maisha ya kuigiza lakini yote ikiwa na lengo moja la kuonyesha ni jinsi gani ambavyo msanii huyo anakabiliana na maisha tofauti tofauti.
Aina ya mchezo huu ni ule mchezo una baadhi ya vipande vya kikubwa, 18+ na vurugu (Dark Drama).
Apple inatoa hela zote za maandalizi ukiachana na yenyewe kuwa katika ushirika mkuu, Dr. Dre pia ni mwandaaji mkubwa kabisa katika matoleo (Episode) 6 ya ‘series’ hiyo. Toleo moja linakadiriwa kuwa na takribani dakika 30 (nusu saa). Pia mastaa wakali kama vile Sam Rockwell na Mo McCrae inasemekana kuwa watakuwa katika mchezo huo wa Tv.
Tukiongelea kiuchumi, Kampuni halipotezi hela kwani ‘Vital Signs’ ni fupi na pia kampuni haitatoa sapoti kubwa – matangazo mengi na gharama zingine kubwa kuhakikisha tamthilia inawalipa – ukilinganisha na Tamthilia za kawaida ya kwenye Tv.
Taarifa zinasema kuwa Tamthilia hii ishaanza kurekodiwa huko Los Angles, California. Na kwa usambazaji kampuni la Apple itaonyesha ‘Series’ nzima kwa wakati mmoja katika mtandao wake wa Apple Music. Ni kitu cha kawaida sana kwa tamthilia za mtandaoni kuachia vipande vyote kwa pamoja.
Ingawa bado kuna taarifa ambazo kidogo bado hazijapata mwangaza kama vile, je Mchezo huu wa kuigiza utaonyeshwa katika Apple Tv au utapatikana katika Stoo ya iTunes? Au hata kuonekana katika Tv za kawaida?.Taarifa hizi wote Apple na msemaji wa Dr. Dre waligoma kuzipa majibu
Taarifa zinazofahamika ni kwamba Tamthilia hii ya Vital Signs itaonyeshwa yote kwa mara moja na moja kwa moja katika mtandao (Streaming) kama vile ilivyo Netflix. Yaani mtu ukitaka kuangalia ni wewe na intaneti yako tuu kwani mzigo mzima utakuwa katika mtandao. Pia kumbuka mchezo huu ni ‘orijino’ kabisa kutoka Apple (Maandalizi na kila kitu)
Fikra zangu ni kwamba ‘Series’ hii itakuwa haiwafai kabisa watoto maana itakuwa na vipande ambavyo havitaendana nao kama vile, vile vya 18+ na vurugu za hapa na pale – Si unajua wamarekani weusi wanavyoigiza? – lakini tusubiri tuone.
No Comment! Be the first one.