Kilichokua kinasubiriwa baada ya tukio la kutambulisha iPhone 14 ni hili la uzinduzi wa Macbook na iPad mpya, habari zilizopo ni kwamba halitakuwepo tena… je ni kitu gani kitafanyika?
Ni wazi kwamba lazima vifaa hivyo vipya viingie sokoni, lakini vitaingia kwa namna yake maana vitatambulishwa bila ya uzinduzi ambao unakua umezoeleka kama kawaida kutoka kwa kampuni ya Apple.

Maswali ni mengi sana juu ya njia gani ambayo wataitumia, kwa taarifa ambayo wameitoa wao wenyewe ni kwamba watotoa bidhaa hizo kimya kimya.
Watakachofanya ni kwamba watatangaza katika majukwaa yao ya mtandaoni lakini hakutakua na uzinduzi ambao tumeuzoea, hata ule wa kimtandao.
Hichi kinafanyika kwa sababu Apple hawana bidhaa nyingi mpya ambazo zitawapelekea kuwa na tukio zima la uzinduzi. Lakini ukifuatilia vizuri hili halitachukiwa na wengi ukilinganisha na bidhaa tajwa.
Ningependa kusikia kutoka kwako niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa Apple kwenda nje ya mfumo wao wa matukio ya uzinduzi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
No Comment! Be the first one.