Kuna App nyingi sana katika soko la App la App Store lakini hizo ni chache sana kulinganisha na zile ambazo hazipo kabisa katika soko hilo.
Kumbuka Apple ndio wana taratibu ngumu kidogo za kufuata mpaka App iingie katika soko hili la App Store ukilinganisha na masoko mengine kama vile Google Play Store.
Apple imeweka wazi dhamira yake ya kutaka kuanza kuruhusu hata App ambazo hazipatikani katika soko laki ziweze kuingia na kutumika katika vifaa vyake.
Kumbuka kipengele hiki kwa Android kina muda murefu na kule kinajulikana kama ‘third part apps’ ambazo una uwezo wa kuziweka katika kifaa cha Android bila kupitia katika soko la App la Android.
Kingine ni kwamba wao Android wanasema kabisa App za aina hii pengine zinaweza zikawa hazina usalama ndani ya kifaa chako maana zinakua zimetoka katika vyanzo vingine ambavyo sio vyao.
Kingine kumbuka kua Apps za aina nyingi, kuna mpaka zile ambazo zinakua zinaelea elewa tuu mfano mzuri ni WhatsApp Web na hizi pia zitakua zina uwezo wa kukaa katika vifaa vya Apple.
Kipengele hiki kwa kipindi cha muda mrefu sana kilikua kinashauriwa sana na watu mbalimbali na hii inaonekana apple wanasikiliza mawazo ya watu.
Mpaka sasa haijulikani ni lini kipengele hiki kitaanza kutumika rasmi katika vifaa vya Apple lakini kwa kasi ya Apple labda ni hivi karibuni kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo katika uwanja wa comment je unadhani ni sawa kwa Apple kuruhusu App za aina hii katika vifaa vyao?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.