Pengine hili linaweza likawa ni geni kabisa kwako, na pia ukizingatia sio mara kwa mara Apple kupitia App store kuwa na tabia ya kuongeza ongeza bei ya Apps.
Maeneo ambayo yataathirika ni nchi nyingi za ulaya, na maeneo mengine, kingine ni kwamba ongezeko hilo la bei za App litaathiri hata bei za manunuzi ya ndani ya App (in-app purchase) zinazopatiakana katika App Store.

Vile vile maeneo kama vile
Chile,
Egypt,
Japan,
Malaysia,
Pakistan,
Poland,
South Korea,
Sweden,
Vietnam,
France,
Germany,
Italy,
Portugal,
Spain.
Na yenyewe yataathirika, ongezeko hilo halijajulikana litakua ni bei gani lakini nahisi itakua ni kulingana na App yenyewe.
Mpaka sasa hakuna maelezo yoyote ambayo yametolewa kuhusiana na Apple kuongeza bei za App katika maeneo hayo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje, unadhani ni sawa kwa kampuni kufanya hivyo?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.