fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao simu Smartphones Teknolojia

Alibaba Watambulisha Teknolojia Ya PAY-WITH-SELFIE!

Alibaba Watambulisha Teknolojia Ya PAY-WITH-SELFIE!

Spread the love
alib

CEO Wa Alibaba Bwn Ma, Akionyesha Jinsi Teknolojia Hii Inavyofanya Kazi

Kutoka na ujio wa kishindo wa Apple Pay na NFC katika iPhone 6 inaonyesha kabisa 2015 utakua ni mwaka ambao malipo kwa kutumia simu (Mobile payments) yataongezeka.

Tayari mamilioni ya watu wanatumia Google Wallet, Paypal na Venmo kulipa bidhaa mbalimbali wanazo nunua katika masoko ya simu/mtandao. Lakini Alibaba anapeleka vitu kwenye sayari nyingine kabisa anapokuja na teknolojia ya “Pay-By-Selfie” yaani lipa kwa kupiga picha ya selfi!

CEO wa Alibaba, Jack Ma, alikua akionyesha teknolojia mabayo inatumia kutambua sura (facial recognition)  ili kutumia kupiga picha ya uso maarufu kama selfie ili kununua vitu katika soko hilo.  Hivi sasa teknolojia hii inafanyiwa majaribio na ‘Ant Financial’, kitengo cha nje cha Alibaba kinachojihusisha na malipo ya mtandaoni

SOMA PIA  India yarusha setelaiti 20 angani kwa mkupuo.

Ma, aliweka wazi katika mkutano wa CeBit  huko mjini Hanover, Ujerumani pale tu alipokuwa anamalizia hutuba yake. Alionyesha watu jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi kwa kumnunulia zawadi meya wa Hanover laivu katika ukumbi.

CEO huyo kwa mbwembwe alibofya kitufe cha “Buy” katika App aliyoiita “Smile to Pay,”  na kujipiga selfie kisha akatangaza kuwa zawadi hiyo itawasilishwa kwa meya huyo baada ya siku 6

SOMA PIA  Ubia wa Huawei na Leica unakaribia kufikia tamati

Ma hakuongea maneno mengi sana na pia siku maalumu ya kuachiwa kwa “Smile to Pay,” bado haijwekwa bayana. Lakini muongeaji wa kike wa kampuni hili aliliambia gazeti la asubuhi la kusini mwa China kuwa kampuni kama kampuni ina msimamo na imejipanga kimkakati kutoa bidhaa (teknolojia) hiyo.

Alibaba tayari ni moja kati ya soko kubwa katika yale yanayolipwa kwa kutumia mtandao (online). AliPay ambayo inafanya kazi kama PayPal tuu ina zaidi ya watu milioni 300 waliojisajili. Wanatoa huduma kwa miamala takribani milioni 80 kwa siku.

SOMA PIA  Undani wa Moto Z4 kwa uchache

Haijawekwa wazi ni baada ya muda gani teknolojia hii inaweza ikaanza kutumika na pia inawezekana kuwa Alibaba sio wenyewe tuu wanaojishughulisha na teknolojia kama hii. Usije ukashangaa kuona Apple na Google wanakuja na bidhaa (teknolojia)  kama hii sokoni

Kumbuka kusambaza makala hiikwa wengine wengi, pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Twitter, Facebook Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania