fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti

Twitter Inafungua Ofisi Dubai!

Twitter Inafungua Ofisi Dubai!

Spread the love

twitter

SAN FRANCISCO — Twitter inafunga ofisi dubai kuwafikia watu wa mashariki ya kati (middle east) kwa urahisi kabisa, katika harakati za kuongeza watumiaji  katika dini hiyo (uislamu)

Kampuni ya Twitter ilitangaza hii habari kupitia tweet iliyotumwa katika mkutano wa ushwawishi wa mitandao ya kijamii (Arab Social Media Influencers Summit) huko mjini Dubai.

“Twitter is coming to Dubai”- akaunti inayotambulika na kuhakikiwa na Twitter Iliandika hivyo

Shailesh Rao, makamu wa raisi wa Twitter upande wa pasifiki ya asia, Amerika ya walatini na Masoko pia ali tweet hii habari

Nguvu kubwa itawekwa katika kuongeza mapato ya matangazo  ndani ya eneo (Dubai) ambapo Twitter ina kama watumiaji milioni 6.

Twitter kama mitandao  mingine ya kijamii kama vile Facebook, imevutiwa kwa kiasi kikubwa sana na mashariki ya kati (middle east).

Kiongozi wa Dubai,Sheikh Mohammed, ana karibia wafuasi (followers) milioni 3.8. Mfalme Salman wa Saudi Arabia ana zaidi ya wafuasi milioni 2.5. Tweet yake ya kwanza aliporudishiwa taji la kuongoza watu wake, watu walii ‘retweet’ mara 260,000 .

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania