fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Intaneti Mtandao wa Kijamii

Twitter Yatimiza Miaka 9!

Twitter Yatimiza Miaka 9!

Spread the love

Siku kama ya leo miaka tisa iliyopita twit ya kwanza kabisa katika mtandao wa Twitter ilitumwa. Twit hiyo ilitumwa na mmoja wa waanzilishi wa mtandao huo Bwana Jack Dorsey, aliandika ya kwamba anaweka sawa akaunti yake ya Twitter.  Alituma Twitter hiyo tarehe 21 mwezi wa tatu mwaka 2006.

TwitterMtandao huo hadi sasa unawatumiaji zaidi ya milioni 500 ila ni takribani watumiaji milioni 285 tuu ndio watumiaji hai – yaani wanaotumia mara kwa mara.

Leo tambua akaunti tano zenye mashabiki wengi zaidi kwa maana ya ‘followers‘ kwenye mtandao huo.

Namba moja ni Mwanamuziki Katy Perry, yeye anazaidi ya ‘followers’ milioni 67

Namba mbili ni Mwanamuziki Justin Bieber, yeye ana followers milioni 61

Namba tatu inashikiliwa na rais Barack Obama wa Marekani, yeye ana followers milioni 56.7

Mwanamziki Taylor Swift ndiye anayeshikilia namba nne. yeye anafollowers milioni 54.6

SOMA PIA  Ongeza Kasi Ya Internet Ya Kompyuta Yako!

Akaunti ya mtandao wa YouTube ndiyo inayoshika namba tano yenyewe ikiwa na followers milioni 49.9

Je nani anaongoza kwa ‘Followers’ Tanzania?

Namba moja inashikiliwa na Rais Jakaya Kikwete, yeye akiwa na followers laki 2.5

Namba mbili inashikiliwa na mwanasiasa maarufu nchini, Bwana Zitto Kabwe, yeye akiwa na followers  laki 2.4

SOMA PIA  Twitter sasa kuhakikisha usalama kwenye mazungumzo

Nafasi ya tatu inashikiliwa na mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Millard Ayo, yeye ana followers laki 2.1

Je wewe unatumia mtandao wa Twitter tokea mwaka gani?

SOMA PIA –  Mambo 20 Kuhusu Mtandao Wa Kijamii Wa Twitter!

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania