fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Tovuti Yahoo

Yahoo! yasogeza mbele mwisho wa kupokea Zabuni

Yahoo! yasogeza mbele mwisho wa kupokea Zabuni

Spread the love

Yahoo! imesogeza tarehe ya mwisho ya kupokea zabuni kutoka kwa wazabuni ambao wana malengo yua kuinunua kampuni hii, badala ya tarehe 11 mwezi huu wazabuni watakuwa na mpaka tarehe 18 kwa mujibu wa vyanzo vilivyoripoti taarifa hii.

Yahoo! ambayo ni kampuni kubwa ya teknolojia ya kimarekani ambayo wengi wanaijua kwa kupitia huduma yake ya barua pepe ambayo ni moja ya mambo yaliyoifanya kampuni hii ifikie mafanikio makubwa zaidi mwaka 2008.

SOMA PIA  Google Chrome na Mozilla Zimeifungia 'KickAss Torrents' Kama Mtandao Wa Udanganyifu!

yahoo

Kutoka mwaka 2008 kampuni hii imekuwa ikifanya vibaya kibiashara na imekuwa ikishuka katika chati, wengi wanainyoshea kidole ushindani ambao uliletwa na kampuni ya Google kuwa ndiyo hasa sababu ya kushindwa kwa Yahoo!. Ingawa yamekuwapo mafanikio ya hapa na pale lakini kimsingi biashara ya kampuni hii ambayo inafanya biashara kama ile inayofanywa na Google imekuwa mashakani kwa kipindi kirefu.

Mwanzoni mwaka huu bodi ya wakurugenzi wa kampuni hii waliamua kuiweka mnadani kampuni hii na kuwataka wateja ambao wana matumaini na kampuni hii kuwasilisha zabuni zao tayari kwaajiri ya kumtafuta mzabuni anayeweza kufikia masharti.

SOMA PIA  Jay Z Atoa Albamu Za 'The Blueprint' Katika Mitandao Mingine Isipokuwa Tidal!

Hatua ya kuiweka kampuni hii katika mnada ilikuwa na kila ishara kwamba bodi ya wakurugenzi hao wamekata tamaa na jitihada za mwanamama Marissa Mayer ambaye amekuwa katika jitihada za kuirudisha kampuni hiyo katika chati lakini jitihada zake zimekuwa tasa.

Yahoo!

Bi. Marissa mayer raisi na mkurugenzi mtendaji Yahoo!

Hii sasa itakuwa ni wiki moja ndefu kwa wadau wakubwa wa Yahoo hasa ambao wamewekeza hisa zao katika kampuni hii kwani baada ya tarehe 18 tutajua ni kampuni gani zitakuwa zimeingia katika mchakato wa kuinunua.

SOMA PIA  ZoomTanzania Yaboresha Soko La Biashara Mtandaoni!

Mpaka sasa tetesi zinaonesha makampuni kadhaa yanaonesha kutaka kuichukua yahoo makampuni hayo ni kama vile Verizon na AT&T ambayo ni makampuni makubwa ya simu nchini marekani.

Makala hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbali mbali katika mtandao hasa CNBC

Comment

Comments

  1. […] post Yahoo! yasogeza mbele mwisho wa kupokea Zabuni appeared first on […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania