Wimbo wa Rhythm Nation wa mwandada Janet Jackson ulitoka mara ya kwanza mnamo mwaka 1989, sasa cha kushangaza ni kwamba inaonakana wimbo huo umeleta ishu ya kiulinzi na kiusalama katika kompyuta za Windows XP.
Hii imerepotiwa na kampuni ya Microsoft kwa kusema kuwa wimbo huo umekua ukileta shida katika baadhi ya computer zinazotumia Windows XP.

Hapa programu endeshaji inayotajwa kabisa ni Windows XP, ikumbukwe pia programu endeshi hiyo kwa sasa haipati sapoti kabisa kutoka katika uongozi wa Microsoft.
Here's our first video from our new series with Raymond Chen, @ChenCravat.
We asked him to tell us about the mystery wherein some music would crash a laptop!!?? pic.twitter.com/BRgfsWEaaC
— Windows Dev Docs (@WindowsDocs) August 12, 2022
Unaweza ukawa unajiuliza sana hivi inawezekanaje kucheza video ya wimbo huo inaweza ikaleta shida kubwa sana katika kompyuta, hapo ndipo teknolojia kwa ujumla itakushangaza.

Injinia wa ‘software’ maarufu wa Microsoft, Raymond Chen, yeye amedai kuwa hiyo kesi imepatika kwa laptop nyingi sana ambazo zinatumia teknolojia ya hard disk ya 5400 RPM.
Bado haiingia akilini sio? Inasemekana kuwa Wimbo huo una masafa (frequency) ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kuharibu hard disk za kompyuta hizo.

Repoti zinasema kuwa kompyuta nyingi tena zile za mfumo wa Notebook ambazo zimekua zikitumia programu endeshi ya Windows hiyo ziliathirika.
Masafa (frequency) hayo yanasemekana kuwa yanafanya kifaa ki’vibrate (kutikisika) pale ambao kinapata nguvu Fulani hivi.
Ni sawa na glasi tuu inaweza ikatikisika na kuvunjika kabisa kama kukiwa na nguvu kubwa ya sauti inayoelekea katika upande wake.

Kingine cha muhimu hapa kufagamu ni kwamba mambo yote haya yalitokea kipindi hicho ambapo Windows XP ndio ilikua imeshika soko sana.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je hata siku moja ulishawahi fikiria kama mziki tuu unaweza ukaharibu kompyuta?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.