WhatsApp bado inazidi kujiimarisha kabisa kwa kuhakikisha kuwa hakuna sababu ambayo itawafanya watumiaji wake kukosa huduma hiyo.
WhatsApp inazidi kujiimarisha na kwa sasa imeweka nia yake ya kuja na kipengele kipya ambacho kitamuwezeza mtumiaji wake kuingia katika akaunti kwa kutumia email (barua pepe)
Uwezo wa kuingia katika mitandao ya kijamii kwa kutumia barua pepe imejaa sana katika mitandao ya kijamii na huwa ndio njia kuu kwa kiasi Fulani.
Hii kwa whatsapp ni nzuri sana maana inawezekana mtu ukawa katika sehemu ambapo hakuna huduma za mitandao ya simu, si unajua ni lazima utumiwe zile kodi kwa njia ya SMS baada ya kuweka namba yako ya simu wakati unaingia katika WhatsApp.
Kingine ni kwamba lazima utahitaji kuwa na namba yako ambayo inahusiana na akaunti hiyo. Hii haimaanishi kwamba hutakua na hutakua na uwezo wa kutumia Email katika kuingia katika akaunti hizo.
Kipengele hiki kikishatoka utaweza kuweka barua pepe (email) yako kwa kuingia katika sehemu ya settings.
Hii ni nzuri sana fikiria kama wewe ni mtu wa kusafiri safari hii inamaana utakuwa na uwezo wa kutumia akaunti moja ya WhatsApp.
Hata ukiwa nchi nyingine utaweza kuingia katika akaunti yako kwa kutumia mtandao mwingine (wa nchi hiyo) huku ukiwa umeacha line yako ndani.
Je unaipa asilimia ngapi whatsapp kwa kufanya uamuzi huu ambao wengi hawakutengemea? ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.