fbpx

apps, Facebook, instagram

Facebook waunganisha uwezo wa kuchati Instagram na Facebook

facebook-waunganisha-uwezo-wa-kuchati-instagram-na-facebook

Sambaza

Facebook waunganisha uwezo wa kuchati Instagram na Facebook. Mara ya kwanza tuliandika kuhusu mpango wa Facebook kuunganisha uwezo wa kuchati na apps zingine za Instagram na WhatsApp mapema mwaka jana. Inaonekana tayari hatua za kuwezesha hilo zimefanikiwa.

Imeripotiwa tayari Facebook inafanya majaribio ya kuwawezesha watumiaji wa Instagram kuweza kuchati na marafiki zao wa Facebook moja kwa moja kwenye app hiyo bila kuhama. Yaani mmoja anakuwa anatuma meseji akiwa Instagram huku anayepokea anapokelea na kujibu akiwa kwenye app ya Facebook Messenger.

Jambo hili linaonekana ni maamuzi ya Facebook kuepuka hatua za kisheria za kulazimisha huduma hizo ziwe makampuni binafsi. Tayari kampuni hiyo ipo kwenye uchunguzi wa kiushindani – Inasemakana kwa Facebook kumiliki app ya Instagram na WhatsApp kunazuia huduma zingine kama hizo kukua/kushamiri.

INAYOHUSIANA  Baada ya siku na miezi kadhaa Apps za HTC zarudi Google PlayStore
kuchati Instagram na Facebook
Kwa watu wa kwanza kupata uwezo huo watagundua watakapotembelea Instagram na kukutana na ujumbe wa kuwezesha/kuunganisha chat za Instagram na zile za Messenger

 

Kwa kufanya hatua za kuunganisha Facebook wanataka kuonesha hizi zote ni huduma moja na hivyo kuja kufanya iwe vigumu vyombo vya serikali hasa vya bara la Ulaya au Marekani kulazimisha kampuni hiyo kujiondoa kwenye umiliki wa WhatsApp na Instagram.

Kwa sasa uwezo huo wa kutuma ujumbe wa maneno, video na picha baina ya watumiaji wa Facebook na Instagram umeanza kupatikana kwa baadhi ya watumiaji wake katika mataifa machache na ni muda wowote kuanzia sasa uwezo huo utasambaa kwa watumiaji wote duniani.

INAYOHUSIANA  Wasimamizi wa makundi Whatsapp kukiona cha moto India
kuchati Instagram na Facebook
Muonekano wa mazungumzo kati ya watumiaji wawili, kushoto mtu akiwa Instagram na kulia ni anayechat naye, yeye akitumia app ya Messenger

Watumiaji wa Facebook Messenger wataweza kupigiana simu za mfumo wa video na wakati huo huo kutazama video za Instagram kwa pamoja.

Hii ni hatua ya kwanza tokea Teknokona iripoti mapema mwaka jana kuhusu uwepo wa mpango huu. Wakuu wa huduma za Instagram na Messenger, Bwana Adam Mosseri na Stan Chudnovsky wamesema kwa kuunganisha huduma hizi watafanya huduma ya kuchati Instagram iwe bora zaidi kufikia vile ambavyo unaweza kuvifanya kwenye app ya Messenger.

INAYOHUSIANA  Whatsapp yaboreshwa; Sasa unaweza kuchora kitu chochote kwenye picha/video

Kujua kama una uwezo wa kufanya hivyo wamesema endelea kuhakikisha unatumia toleo la kisasa zaidi la Instagram kwa kusasisha app hiyo.

Je una mtazamo gani kuhusu jambo hili? Facebook wanasema muda si mrefu uwezo huo utapatikana kwa watumiaji wote, na pia tayari wanafanyia kazi jinsi ya kuuleta kwa watumiaji wa WhatsApp pia.

Chanzo: TheGuardian.com, CNN na vyanzo mbalimbali
Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*