WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambao ni pendwa na ni maarufu sana, ni moja kati ya njia za mawasiliano za haraka sana.
Kwa sasa mtandao huo — WhatsApp — uko katika mchakato wa kuanzisha kipengele cha kuona mara moja tuu meseji ambayo mtu katuma.
Ni wazi kuwa katika kipengele hiki kwa sasa hakipo katika upande wa meseji lakini kipo kama utakua na mpango wa kutuma picha au video.
Ukiwa unatuma mafaili ya namna hiyo ndio utaweza kuamuru unaemtumia aweze kuona kwa mara moja tuu na kisha mafaili hayo kujifunga na kujifuta kabisa.
Kipengele hiki ni kizuri kikija katika meseji za kawaida pia maana kuna watu wanatumiana meseji lakini baadae huwa wanazifuta kabisa meseji hizo.
Ukiachana na hao, kuna wengine ndani ya mtandao huu wameweka kabisa muda maalamu wa meseji zao kufutika zenyewe kila baada ya muda Fulani wengi ikiwa ni masaa 24.
Kwa sasa kipengele hiki kinaweza kupatikana kupitikana kwa watu wachache sana ambao wamechaguliwa kuwa kama sehemu ya majaribio ya kipengele hicho.
Kupitia toleo hilo la majaribio (beta) ukiwa umetuma meseji kwa mfumo huo wa kupotea –view once — basi mtu anaetuma na anaetumiwa wote wawili meseji hiyo itafutika mara tuu baada ya alietumiwa kuisoma.
Pengeine hakutakua na tofauti kabisa katika uwezeshaji wa kipengele hiki kufanya kazi, pengine hakutakua na utofauti kabisa na kile cha picha/video zinazopotea baada ya kuziangalia tuu.
Ili kupata vipengele vipya vya mtandao wa WhatsApp ni lazima kuhakikisha kuwa una toleo la juu kabisa (sasisho/update) hivyo hakikisha kifaa chako kina toleo hilo.
Chanzo: WABetaInfo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unatafurahia kuanza kutumia huduma hii au huna mpango nacho kabisa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.